Benki ya Deutsche ya Ujerumani kufunga akaunti za Donald Trump
Benki kubwa ya Deutshe nchini Ujerumai imetangaza kuwa itazifunga akaunti za Rais wa Marekani Donald Trump kufuatia matukio yaliyojiri karibui katika Kongresi ya Marekani.
Tovuti ya habari ya Bloomberg imeripoti kuwa, baada ya matukio ya kushambuliwa Kongresi ya Marekani, viongozi wa Benki ya Deutsche ya Ujerumani wametangaza kuwa benki hiyo imeamua kusitisha miamala ya kibiashara ya Rais Donald Trump wa Marekani na taasisi yake. Rais wa Marekani anadaiwa zaidi ya dola milioni 300 na benki hiyo ya Ujerumani yenye makao yake huko Frankfurt.
Benki ya Deutsche ambayo taswira yake imeharibika kutokana na miamala yake ya kibiashara na Rais Donald Trump katika kampeni za uchaguzi miaka minne iliyopita, imelazimika pia kuwafukuza wafanyakazi wake elfu 18 kutokana na hasara ya fedha iliyopata.
Wafuasi wa Rais Donald Trump wa Marekani Jumatano iliyopita tarehe 6 Januari walishambulia Kongresi ya nchi hiyo kwa masaa kadhaa na kuidhibiti. Raia wasiopungua 5 akiwemo polisi moja waliuawa katika shambulio hilo. Wawakilishi wa chama cha Democratic tayari wameanzisha mchakato wa kusailiwa na kuuzuliwa Trump baada ya kujiri shambulio hilo.