Pars Today
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, watu zaidi ya milioni 7.3 wamepatwa na ugonjwa wa Malaria nchini Ethiopia huku wagonjwa 1,157 wakiaga dunia kwa ugonjwa huo kuanzia Januari Mosi hadi Oktoba 20 mwaka huu.
Katika mkutano muhimu wa kidiplomasia, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amekutana na Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia, ambapo wamejadili masuala muhimu ya pande mbili na kikanda.
Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa Mkataba wa Ushirika wa Bonde la Mto Nile (CFA) ulianza kutekelezwa rasmi jana Jumapili licha ya Misri na Sudan kuendelea kuupinga.
Karibu watu 37 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kaskazini mwa Ethiopia, ambapo maporomoko ya ardhi na mafuriko yameharibu maeneo mengi ya ukanda huo.
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika eneo la kaskazini la Amhara nchini Ethiopia zimewaweka watu 400,000 katika hatari ya mafuriko na maporomoko ya ardhi.
Takriban watu 16,000 wamelazimika kuhama makazi yao na kuelekea katika maeneo salama kutokana na mafuriko yaliyoathiri maeneo ya magharibi mwa Ethiopia.
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha huko mashariki mwa Sudan imezidisha mateso ya watu waliokimbia makazi yao haswa katika miji ya Gedaref, Kassala na Halfa Aj Jadeedah.
Bunge la Ethiopia limetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Jumamosi kufuatia maporomoko ya udongo yaliyoua mamia ya watu.
Watu wasiopungua 229 wamepoteza maisha katika maporomoko ya udongo yaliyoikumba Ethiopia baada ya mvua kubwa kunyesha nchini humo.
Spika wa Bunge la Ethiopia amesema aghalabu ya nchi za Afrika zina hamu ya kuwa wanachama wa kundi la BRICS la mataifa yanayoinukia kiuchumi duniani.