Pezeshkian: BRICS inatoa fursa ya ushirikiano imara zaidi wa wanachama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i134278-pezeshkian_brics_inatoa_fursa_ya_ushirikiano_imara_zaidi_wa_wanachama
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameashiria nafasi na uwezo wa kundi la BRICS na kulieleza kama jukwaa muhimu la kuimarisha maingiliano na uhusiano wa kiuchumi na kisiasa miongoni mwa nchi wanachama.
(last modified 2025-12-14T02:53:50+00:00 )
Dec 14, 2025 02:53 UTC
  • Pezeshkian: BRICS inatoa fursa ya ushirikiano imara zaidi wa wanachama

Rais Masoud Pezeshkian wa Iran ameashiria nafasi na uwezo wa kundi la BRICS na kulieleza kama jukwaa muhimu la kuimarisha maingiliano na uhusiano wa kiuchumi na kisiasa miongoni mwa nchi wanachama.

Rais Pezeshkian alisema hayo katika mkutano na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Ethiopia Tagesse Chafo mjini Tehran jana Jumamosi na kuilezea BRICS kama mfumo mpya wa mawasiliano unaokuza heshima kwa uhuru wa kitaifa na tamaduni mbalimbali, na kufungua njia ya ushirikiano wa usawa wa kimataifa.

Pezeshkian ameelezea nia ya Iran ya kuendeleza uhusiano wa pande mbili na Ethiopia, akisisitiza kwamba kufikia lengo hili kunahitaji kuanzishwa kwa tume ya ushirikiano wa pamoja, kutambua maslahi ya pamoja, kutambua uwezo wa kukamilishana, na kukuza mazungumzo yenye kuzingatia maslahi ya pande zote mbili.

Rais Pezeshkian amesisitiza utayari wa Iran kuchukua jukumu la uwajibikaji katika kuanzisha na kuimarisha amani na usalama endelevu katika eneo, akitoa mwito wa kuwa na ulimwengu usio na vita, vurugu, na migogoro. Amesema anaamini kwamba, watu binafsi wenye ufahamu wa kina kuhusu asili ya binadamu wanapendelea mazungumzo na ushirikiano kuliko makabiliano.

Maspika wa Mabunge ya Iran na Ethiopia katika mazungumzo Tehran

Wakati wa mkutano huo, Spika wa Ethiopia alielezea kuridhika kwake na majadiliano hayo na kusisitiza kujitolea kwa Ethiopia kuimarisha uhusiano na Iran, haswa katika sekta za kidiplomasia, kiuchumi, na usalama.

Kabla ya hapo, Spika wa Bunge la Iran Mohammad Bagher Ghalibaf katika mkutano wake na Spika huyo wa Ethiopia alisema Tehran na Addis Ababa zina azma ya kupanua uhusiano wao wa kisiasa, kiuchumi, na kitamaduni, huku uanachama wa hivi karibuni wa nchi zote mbili wa BRICS ukitarajiwa kurahisisha ushirikiano wa karibu zaidi,

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Ethiopia, Tagesse Chafo katika Bunge la Iran jana Jumamosi, Ghalibaf alisema uhusiano wa muda mrefu wa mataifa haya mawili ni wa zaidi ya miongo 7.