-
Addis Ababa: Hakuna askari yeyote wa Ethiopia aliyekuwa mateka nchini Sudan
Apr 22, 2021 03:22Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ethiopia amesema Sudan imeikabidhi nchi hiyo wakulima 59 na wanamgambo wawili wa kieneo.
-
Ethiopia: File na bwawa la Renaissance si kadhia ya kimataifa
Apr 16, 2021 07:36Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ethiopia amepinga mpango wowote wa kulifanya suala la bwawa la Renaissance kuwa mgogoro wa kimataifa.
-
UN: Eritrea ikomeshe ukatili na mauaji Tigray
Apr 16, 2021 07:35Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, askari wa Eritrea wanapaswa kukomesha ukatili na vitendo viovu katika eneo la Tigray nchini Ethiopia na kuondoka mara moja katika eneo hilo.
-
Amnesty: Jeshi la Eritrea linaendelea kuua raia Tigray, Ethiopia
Apr 15, 2021 23:04Shirika la kutetea haki za binadamu la Amesty International limesema jeshi la Eritrea lingali linaua raia katika eneo la Tigray, wiki chache baada ya Ethiopia kutangaza kuwa wanajeshi wa nchi hiyo jirani yake wameanza kuondoka katika eneo hilo linalokumbwa na mgogoro na mapigano kwa miezi kadhaa sasa.
-
Ethiopia inakabiliwa na uhaba wa mitungi ya oxygen kwa ajili ya wagonjwa wa corona
Apr 13, 2021 07:26Moja ya viwanda vikubwa vya kutengeneza oxygen nchini Ethiopia ambavyo kwa siku hudhamini zaidi ya mitungi elfu mbili ya hewa ya oxygen kwa ajili ya wagongwa wa corona nchini humo kimekumbwa na matatizo ya kiufundi.
-
Sudan: Hakuna ufumbuzi wa kijeshi wa mgogoro wa bwawa la Renaissance
Apr 09, 2021 08:57Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Sudan amesema kuwa, ni jambo lililo mbali kwamba mgogoro wa bwawa la Renaissance unaweza kutatuliwa kwa njia za kijeshi ili kuizuia Ethiopia kuendeleza mradi ujenzi wa bwawa hilo juu ya maji ya Mto Nile.
-
Kushindwa mara kadhaa mazungumzo kuhusu bwawa la An Nahdhah; Misri yatoa vitisho
Apr 08, 2021 22:08Mazungumzo ya kuainisha suala la maji ya bwawa la An Nahdhah na kuanza marhala ya pili ya uingizaji maji bwawani kwa mara nyingine tena yamegonga mwamba; na kumalizika bila ya natija yoyote huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Baada ya kufeli mazungumzo hayo, Misri imeitishia Ethiopia kwamba itachukua hatua.
-
Rais wa Misri aonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita na Ethiopia
Apr 08, 2021 03:08Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri ameionya Ethiopia kuhusu kutokea vita baina ya nchi hizo mbili iwapo Addis Ababa itaendelea kushikilia msimamo wake wa kuingiza maji katika bwawa la al Nahdha.
-
Wafugaji 100 wauawa katika mapigano ya kugombania ardhi Ethiopia
Apr 07, 2021 03:15Mapigano baina ya wafugaji wa jamii hasimu zinazopakana katika eneo la Afar na Somali kaskazini mashariki mwa Ethiopia yamepelekea watu zaidi ya 100 kuuawa.
-
Ethiopia yaalani taarifa ya kundi la G-7 kuhusu eneo la Tigray
Apr 06, 2021 22:31Ethiopia imelaani na kukosoa taarifa iliyotolewa katika kikao cha kundi la G-7 kuhusu hali ya mambo katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo.