Ethiopia yaalani taarifa ya kundi la G-7 kuhusu eneo la Tigray
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i68748-ethiopia_yaalani_taarifa_ya_kundi_la_g_7_kuhusu_eneo_la_tigray
Ethiopia imelaani na kukosoa taarifa iliyotolewa katika kikao cha kundi la G-7 kuhusu hali ya mambo katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 06, 2021 22:31 UTC
  • Ethiopia yaalani taarifa ya kundi la G-7 kuhusu eneo la Tigray

Ethiopia imelaani na kukosoa taarifa iliyotolewa katika kikao cha kundi la G-7 kuhusu hali ya mambo katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imetoa taarifa na kutangaza kuwa, taarifa iliyotolewa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za kundi la G-7 linaloundwa na Marekani, Canada, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, ,Italia na Japan katika kubainisha hatua muhimu zilizochukuliwa na serikali ya Ethiopia kwa ajili ya kuandaa mahitaji ya dharura kwa ajili ya eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo ambazo zimetekelezwa kikamilifu, imegonga mwamba. 

Nchi za G-7 zimetaka wanajeshi wa Eritrea waondoke haraka iwezekanavyo na bila ya masharti yoyote katika eneo la Tigray; ambapo serikali ya Ethiopia katika taarifa yake imetangaza kuwa, wanajeshi wa Eritrea tayari wameondoka katika eneo hilo kaskazini mwa Ethiopia, na kwamba vikosi vya ulinzi wa taifa vya nchi hiyo hivi sasa ndivyo vinavyolinda mipaka ya Ethiopia. 

Eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imetangaza mashirika ya masuala ya kibinadamu sasa yamepewa jukumu la kulifikia kikamilifu, na hivi karibuni kutaanza kufanyika uchaguzi wa pamoja na wataalamu kutoka nje kuhusu madai ya ukiukaji wa haki za binadamu huko Tigray. Mwanzoni mwa mwezi Machi mwaka huu Shirika la Amnesty International lililituhumu jeshi la Eritrea kuwa limefanya mauaji ya umati katika eneo la Tigray.