-
Mzozo kati ya Ethiopia na Somalia wazidi kuongezeka
Apr 10, 2024 03:04Tangu kutangazwa kwa makubaliano ya bahari kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland miezi mitatu iliyopita, hali ya mvutano imekuwa ukiendelea kati ya nchi hizo mbili jirani za mashariki mwa Afrika na washirika wa usalama.
-
Somalia yamtimua balozi wa Ethiopia kutokana na mgogoro wa mkataba wa bandari ya Somaliland
Apr 05, 2024 02:20Somalia imetangaza kumfukuza balozi wa Ethiopia nchini humo huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kuhusu mzozo wa makubaliano ya bandari kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland.
-
Wabunge wa Somaliland wafutilia mbali makubaliano na Ethiopia ya kufika Bahari Nyekundu
Feb 15, 2024 07:47Wabunge katika eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland wamefutilia mbali makubaliano waliyofikia na Ethiopia ya kuiruhusu Addis Ababa kutumia bandari kuu katika eneo la Somaliland.
-
Jeshi la Ethiopia latuhumiwa kuua makumi ya raia jimboni Amhara
Feb 14, 2024 07:35Kamisheni ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia (EHRC) imedai kuwa wanajeshi wa serikali ya Ethiopia waliwaua raia wasiopungua 45 wa mji wa Merawi katika jimbo la Amhara la kaskazini mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Bunge la Ethiopia larefusha 'hali ya hatari' eneo la Amhara
Feb 03, 2024 07:28Bunge la Ethiopia jana Ijumaa lilirefusha muda wa hali ya hatari iliyotangazwa Agosti mwaka uliopita 2023 katika eneo linaloshuhudia mapigano la Amhara.
-
Watu 225 wapoteza maisha kutokana na makali ya njaa Tigray, Ethiopia
Jan 17, 2024 07:41Watu wasiopungua 225 wameaga dunia katika eneo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia kutokana na njaa iliyosababishwa na ukame ambao umeendelea kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
-
OIC yataka kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala Somalia
Jan 05, 2024 02:32Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa mwito wa kuheshimiwa mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi yote ya Somalia, kufuatia kusainiwa mapatano baina ya Ethiopia na Somaliland yatakayoiwezesha Ethiopia kutumia Bandari ya Berbera ya Somalia iliyoko katika eneo hilo la Somaliland.
-
Ethiopia yatia saini makubaliano ya bandari ya kihistoria na Somaliland
Jan 02, 2024 03:27Ethiopia imefikia makubaliano ya kihistoria ya kutumia bandari kuu katika eneo lililojitenga la Somalia, la Somaliland wakati nchi hiyo isiyo na eneo lililoungana na bahari ikitafuta ufikiaji zaidi wa njia za baharini kwa meli. Haya yalibanishwa jana na maafisa wa pande mbili.
-
Njaa yaua watu 176 eneo la Tigray, Ethiopia
Dec 14, 2023 03:10Watu wasiopungua 176 wameaga dunia katika eneo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia kutokana na njaa iliyosababishwa na ukame ambao umeendelea kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
-
Idadi ya waliofariki kutokana na mripuko wa kipindupindu nchini Ethiopia yafikia watu 400
Dec 02, 2023 10:33Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limetangaza kuwa, mripuko wa kipindupindu unaoendelea nchini Ethiopia, hadi hivi sasa umeshasababisha vifo vya zaidi ya watu 400 kufikia sasa.