-
Ethiopia kuzindua awamu ya nne ya ujazaji maji katika bwawa lenye mvutano
Jun 23, 2023 04:03Ethiopia inajiandaa kuanzisha awamu ya nne ya kujaza maji katika hifadhi ya bwawa lake kubwa katika Blue Nile. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo licha ya upinzani wa jirani yake Misri.
-
Ethiopia yawatimua Waganda waliohadaiwa kwenda 'kuonana' na Yesu
Jun 13, 2023 03:57Mamlaka za Ethiopia zimewarejesha nyumbani raia 80 wa Uganda ambao walitapeliwa fedha zao kwa ahadi kwamba watapelekwa kukutana na Yesu katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Ethiopia yapinga tuhuma za maangamizi ya kizazi huko Tigray Magharibi
Jun 07, 2023 07:00Serikali ya Ethiopia imepinga ripoti iliyotolewa na Shirika la Haki za Binadamu la (HRW) iliyodai kuwa kampeni ya maangamizi ya kizazi imefanyika huko Tgray Magharibi licha ya kutiwa saini makubaliano ya amani mwezi Novemba mwaka jana.
-
Wawili wauawa katika maandamano ya kupinga kubomolewa misikiti zaidi ya 19 Ethiopia
May 27, 2023 07:19Watu wawili wameuawa wakati askari polisi walipowashambulia Waislamu walioandamana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kupinga kubomolewa misikiti yao zaidi ya 19 katika eneo la kandokando ya mji huo.
-
Waasi wa Oromo wa Ethiopia wavituhumu vikosi vya serikali kwa kufanya mashambulizi
May 17, 2023 21:37Waasi katika jimbo la Oromia nchini Ethiopia wameituhumu serikali kuu ya nchi hiyo kuwa imefanya mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi yao baada ya mazungumzo ya amani kati ya pande mbili kumalizika bila kufikia mapatano.
-
Makumi watiwa nguvuni Ethiopia baada ya mauaji ya afisa wa chama tawala
May 01, 2023 03:40Askari usalama wa Ethiopia wametangaza kuwa wamewakamata watu 47 kufuatia mauaji ya afisa wa chama tawala nchini humo.
-
WFP inachunguza wizi wa chakula cha msaada nchini Ethiopia
Apr 11, 2023 22:42Shirika la Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) linachunguza wizi wa misaada ya chakula ulioripotiwa katika oparesheni za kibinadamu huko Ethiopia.
-
Ethiopia kuunganisha vikosi vya majimbo ya kikanda katika jeshi la taifa na polisi
Apr 10, 2023 08:05Serikali ya Ethiopia imesema kuwa inakusudia kujumuisha vikosi vyote maalumu vya majimbo ya kikanda ima katika jeshi la taifa, au polisi ya shirikisho au majimbo; hatua ambayo inaweza kuhesabiwa kama mpango wa kuyapunguzia mamlaka majimbo yanayosimamia mambo yake yenyewe.
-
Hafla kubwa zaidi ya futari yafanyika Ethiopia
Apr 09, 2023 08:00Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Ethiopia limefanya hafla kubwa zaidi ya Iftar katika uwanja wa Al-Thaura mjini Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo, wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Ethiopia yaunda serikali ya mpito katika eneo la Tigray
Mar 24, 2023 03:40Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ametangaza habari ya kuundwa serikali ya mpito katika eneo la Tigray la kaskazini mwa nchi, kama sehemu ya utekelezaji wa makubakubaliano ya amani.