-
Meja Jenerali Jaafari: Ujumbe wa Iran kwa nchi za Ghuba ya Uajemi ni wa amani na urafiki
Sep 05, 2018 09:21Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, ujumbe wa Iran kwa nchi za Ukanda wa Ghuba ya Uajemi ni wa amani na urafiki sambamba na kuleta hali ya ushirikiano kwa ajili ya kudhamini amani katika maji ya Ghuba ya Uajemi bila ya uwepo wa vikosi vya madola ajinabi.
-
Meja Jenerali Bagheri: Maadui ni walowezi Ghuba ya Uajemi
Aug 29, 2018 21:56Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kutokana na uimara wa kikosi cha majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH), nchi maadui huwa zina woga mkubwa kabla ya kuingia katika Lango Bahari la Hormoz (la kusini mwa Iran) na katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, maadui hao wamelazimika kuheshimu sheria za kimataifa.
-
Marekani imebakia kuangalia kwa macho tu uwezo wa kijeshi wa Iran Ghuba ya Uajemi
Aug 09, 2018 09:10Kamanda wa Komandi Kuu wa Jeshi la Marekani amezungumzia luteka mazoezi ya kijeshi yaliyoifanywa hivi karibuni na Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormoz na kukiri uwezo mkubwa wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rais Rouhani: Wanaolitakia mabaya taifa la Iran muda si mrefu watasailimu amri
Jun 28, 2018 09:06Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, kuna haja ya kukabiliana na vitisho vya adui na kuvibadilisha kuwa fursa, kwani wanaolitakia mabaya taifa hili muda si mrefu watasalimu amri.
-
Waislamu duniani wanaswali Swala ya Iddi Ijumaa ya leo
Jun 15, 2018 00:21Waislamu katika nchi mbalimbali duniani leo wanaswali Swala ya Iddil-Fitri baada ya kutangazwa kuonekana kwa mwezi mwandamo na kukamilika mwezi wa Ramadhan.
-
Mwanaharakati wa Kisiasa Kuwait: Saudia ndio muharibifu wa usalama Mashariki ya Kati
May 01, 2018 09:44Mwanaharakati mashuhuri wa kisiasa nchini Kuwait amesambaza video inayoonyesha kuwa Saudia ndiye muhusika mkuu wa machafuko eneo la Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati kwa ujumla.
-
"Ghuba ya Uajemi" (Persian Gulf); Jina Litakalobaki Milele Katika Kurasa za Historia
May 01, 2018 04:05Ni matumaini yangu kuwa hujambo mpenzi msikilizaji popote pale ulipo. Jumatatu ya tarehe 30 Aprili ilisadifiana na siku ya mwisho ya kuondoka Wareno baada ya kutimuliwa kwenye eneo la maji ya kusini mwa Iran. Kwa mnasaba wa tukio hilo, siku hii inajulikana katika kalenda rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama "Siku ya Taifa ya Ghuba ya Uajemi". Baada ya utangulizi huo mfupi nakuomba sasa ujiweke tayari kusikiliza yale niliyokuandalia kwa mnasaba wa siku hiyo.
-
Jumatatu, tarehe 30 Aprili, 2018
Apr 29, 2018 23:17Leo ni Jumatatu tarehe 13 Shaaban, 1439 Hijria sawa na Aprili 30, 2018 Miladia.
-
Qatar: Saudia inayakandamiza 'mataifa madogo' kwa lengo la kuyapigisha magoti
Nov 18, 2017 04:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema utawala wa Saudi Arabia unachochea migogoro na mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati sambamba na kuzikandamiza na kuzinyanyasa nchi ndogo katika eneo ili kuzishinikiza zipige magoti mbele yake.
-
Sayyari: Tamko la kipumbavu la Trump haliwezi kubadilisha "Ghuba ya Uajemi"
Oct 17, 2017 23:19Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Majini cha Iran amesema kauli ya kupotosha na ya kipumbavu iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani alipokuwa akitoa hutuba dhidi ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hivi karibuni haiwezi kubadilisha jina la asili la "Ghuba ya Uajemi".