Sayyari: Tamko la kipumbavu la Trump haliwezi kubadilisha "Ghuba ya Uajemi"
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i35774-sayyari_tamko_la_kipumbavu_la_trump_haliwezi_kubadilisha_ghuba_ya_uajemi
Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Majini cha Iran amesema kauli ya kupotosha na ya kipumbavu iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani alipokuwa akitoa hutuba dhidi ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hivi karibuni haiwezi kubadilisha jina la asili la "Ghuba ya Uajemi".
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 17, 2017 23:19 UTC
  • Sayyari: Tamko la kipumbavu la Trump haliwezi kubadilisha

Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Majini cha Iran amesema kauli ya kupotosha na ya kipumbavu iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani alipokuwa akitoa hutuba dhidi ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hivi karibuni haiwezi kubadilisha jina la asili la "Ghuba ya Uajemi".

Admeli Habibollah Sayyari aliyasema hayo jana Jumanne mjini Venice nchini Italia, ambako anahudhuria Warsha ya Kieneo ya Majeshi ya Majini ya Nchi Zinazopakana na Bahari ya Mediterraenian na Bahari Nyeusi na kuongeza kuwa, kuna haja Trump apewe kozi ya jografia na kisha azungumze kama rais wa nchi.

Admeli Sayyari amebainisha kuwa, kitendo cha Trump cha kusema neno Ghuba ya Arabu badala ya Ghuba ya Uajemi katika hotuba yake ni ishara tosha kuwa hana uelewa wala ufahamu wowote juu ya masuala ya jografia na historia.

Rais Trump wa Marekani

Siku ya Ijumaa iliyopita, Trump alizindua stratijia mpya ya Marekani kuhusu Iran ambapo alikataa kuidhinisha kuwa Iran inatekeleza na mapatano ya nyuklia ambayo yanajulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA). Hatua hiyo imekosolewa vikali ndani na nje ya Marekani.

Hivi karibuni, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton alisema hatua ya Trump ya kutaka kuvuruga mapatano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 ni jambo ambalo limeifanya Marekani ionekane kuwa nchi duni, ya kijinga na ambayo haiwezi kuaminika katika uga wa kimataifa.