Waislamu duniani wanaswali Swala ya Iddi Ijumaa ya leo
(last modified Fri, 15 Jun 2018 04:51:06 GMT )
Jun 15, 2018 04:51 UTC
  • Waislamu duniani wanaswali Swala ya Iddi Ijumaa ya leo

Waislamu katika nchi mbalimbali duniani leo wanaswali Swala ya Iddil-Fitri baada ya kutangazwa kuonekana kwa mwezi mwandamo na kukamilika mwezi wa Ramadhan.

Hii ni baada ya nchi mbalimbali kuanzia Asia, Afrika na maeneo mengine ya duania kutangaza jioni ya jana konekana mwezi mwandamo wa Shawwal 1439 Hijiria. Miongoni mwa nchi zinazoswali Swala ya Iddi asubuhi ya leo ni pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Saudi Arabia, Qatar, Oman, Lebanon, Palestina, Jordan, Kuwait, Imarati, Bahrain, Tanzania, Kenya, Burundi, Uganda  na kadhalika. Kwa mnasaba huo serikali za mataifa hayo zimetangaza likizo ya siku kadhaa ambapo baadhi zimetangaza likizo ya siku nne hadi 12.

Kiongozi Muadhamu akiwahutubia Waislamu baada ya swala ya Iddi mapema leo

Katika dini ya Uislamu tarehe Mosi Shawwal inajulikana kama siku ya Iddil-Fitri ambamo ndani yake Waislamu husherehekea kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan, ambao ndani yake hujipinda katika kufanya ibada na kuomba msamaha wa dhambi zao. Mjini Tehran ibada ya Swala ya iddi imeongozwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei. Katika siku hii ya ya Idi Waislamu wanatakiwa kujiepusha na maasi na kuswali Swala ya iddi,  kuwasaidia watu masikini, kuwatembelea wagonjwa, kuwasaidia na kuwazuru watoto mayatima na ibada nyinginezo.

Redio Tehran inatoa mkono wa Idul Fitri kwa Waislamu kote duniani hususan wasikiliza na wafuatiliaji wa matangazo yetu.