Aug 07, 2023 12:04
Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amelaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria na kusababisha vifo vya askari wanne wa nchi hiyo na kusisitiza kuwa, umma wote wa Kiislamu unapaswa kuungana pamoja kukabiliana na utawala huo dhalimu.