White House yakiri kuhusu nafasi muhimu ya Hamas
https://parstoday.ir/sw/news/world-i119618-white_house_yakiri_kuhusu_nafasi_muhimu_ya_hamas
Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani amekiri kuhusu nafasi muhimu ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika eneo.
(last modified 2024-12-02T11:58:39+00:00 )
Dec 02, 2024 11:58 UTC
  • White House yakiri kuhusu nafasi muhimu ya Hamas

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani amekiri kuhusu nafasi muhimu ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika eneo.

Jack Sullivan ameeleza kuwa harakati ya Hamas hivi sasa ndiyo upande mkuu katika mapatano ya kusitisha vita yanayoweza kufikiwa kati yake na Israel na kwamba harakati hiyo ina nafasi muhimu katika suala la kubadilishana mateka. 

Karibu mateka 250 wa utawala wa Kizayuni  wanashikiliwa na wanamuqawama wa Palestika katika Ukanda wa Gaza. 

Wakati huo huo, familia za mateka hao wa Kizayuni zinasisitiza kuwa, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ndiye anayehusika na maisha ya mateka hao wa Israel ambaye anaendelea kushadidisha vita kwa kupuuza hatima ya ndugu zao.  

Hii ni katika hali ambayo idadi kadhaa ya mateka wa Kizayuni wa Israel wameuliwa huko Gaza kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika eneo.