Wanajeshi wa Kizayuni waangamizwa Gaza na wanamuqawama wa HAMAS
(last modified 2024-10-14T11:37:25+00:00 )
Oct 14, 2024 11:37 UTC
  • Wanajeshi wa Kizayuni waangamizwa Gaza na wanamuqawama wa HAMAS

Wanajeshi kadhaa wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa na kujeruhiwa na Mujahidina wa Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Qassam imesema wapiganaji wake wameripua kifaa katika shambulio hilo dhidi ya wanajeshi wa Israel, walipokuwa wakijaribu kuingia katika nyumba moja kusini mwa mji wa Gaza.

Kanali ya televisheni ya al-Jazeera imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, tukio hilo katika kitongoji cha al-Janaina mashariki mwa Rafah limeua na kujeruhi idadi kubwa ya wanajeshi wa Kizayuni.

Katika tukio jingine tofauti, wapiganaji wa Izzuddin Qassam walishambulia na kuharibu vifaru viwili aina ya Merkava vya Israel kwa kutumia maroketi ya Yassin katika kitongoji kimoja kusini mwa Gaza.

Askari wa Israel wala kichapo kutoka wanajihadi wa Qassam

Utawala wa Kizayuni unaendelea kupuuza miito ya jamii ya kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kuutaka usimamishe vita mara moja, na pia amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)  ya kuutaka uchukue hatua za kuzuia mauaji ya kimbari katika Ukanda wa  Gaza.

Idadi ya mashahidi katika Ukanda wa Gaza imepundukia watu elfu 42,300 na waliojeruhiwa ni zaidi ya 98,000, tangu kuanza kwa Operesheni ya Kimbunga cha  al-Aqsa.

 

Tags