-
Somalia: Imarati inaunga mkono makundi ya wabeba silaha na kuchochea machafuko
Oct 15, 2026 02:45Waziri wa Ulinzi wa Somalia, Ahmed Moallim Fiqi, ameituhumu Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuingilia mambo ya ndani ya Somalia, kuchochea migawanyiko ya kisiasa na kuwaunga mkono viongozi wa upinzani wanaoipinga Serikali ya Shirikisho. Tuhuma hizo zimeibuka wakati kukiwa na maonyo kuhusu uhamasishaji wa makundi yenye silaha unaotishia usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
-
Imarati na Israel zapapurana, safari za ndege zapigwa marufuku
Oct 06, 2026 03:08Shirika la usalama wa ndani la Israel limepinga uendeshaji wa safari za ndege kutoka Dubai kwenda Tel Aviv zilizokusudiwa kuwarejesha abiria wa utawala wa Kizayuni waliokwamba Dubai.
-
Netanyahu ametembelea UAE, amekutana na wawakilishi wa Saudia, Qatar, Jordan, Libya, Morocco
Sep 29, 2026 10:30Ofisi ya waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu, imethibitisha kuwa yeye na mkewe Sara, walisafiri hadi Muuungano wa Falme za Kiarabu (UAE) siku ya Jumapili kwa mwaliko wa rais wa nchi hiyo Mohammed bin Zayed.
-
Iran yakanusha madai kuwa imeishambulia UAE kwa makombora
Aug 19, 2026 04:18Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha vikali madai ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwamba Iran imevurumisha makombora mawili ya balestiki kuelekea nchi hiyo.
-
Khartoum yatoa ushahidi dhidi ya UAE na kuikosoa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai
Jul 18, 2026 09:07Waziri wa Sheria wa Sudan, Abdullah Darf, amewasilisha kifurushi cha njia za kisheria "zisizo za kawaida" ambazo serikali ya Khartoum inakusudia kuchukua ili kufungua mashtaka dhidi ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kundi la waasi la Rapid Support Forces (RSF), akisisitiza kwamba Khartoum ina "ushahidi wa kutosha na data kamili" kuhusu "ushiriki wa Abu Dhabi katika vita na uhalifu uliofanywa na pande hizo mbili dhidi ya watu wa Sudan."
-
Watetezi haki za binadamu: NBA ikomeshe ushirikiano na UAE katika mauaji ya halaiki Sudan
Jun 03, 2026 13:10Watetezi wa haki za binadamu wamekitaka Chama cha Kitaifa cha Mpira wa Kikapu cha Marekani (NBA) kukomesha ushirikiano wake na Umoja wa Falme za Kiarabuu (UAE), wakisema uhusiano wa ligi hiyo na Abu Dhabi unaikingia kifua nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi kutokana na kulaaniwa vikali kwa kuhusika kwake katika vita ndani nchini Sudan.
-
MEE: Misri iliishinikiza Al-Azhar 'kuunga mkono UAE' katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran
May 23, 2026 02:43Ripoti zinasema kwamba Ofisi ya Rais wa Misri iliishinikiza taasisi ya Al-Azhar, ambayo ni mamlaka ya juu zaidi ya Waislamu wa madhehebu ya Suni, kuunga mkono hadharani Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na mataifa mengine ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
-
Kushiriki UAE katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran ni 'haramu kabisa'
May 13, 2026 12:18Chuo Kikuu cha Kimataifa cha al-Mustafa kimetangaza kuwa ushiriki, uwezeshaji na ushirikiano wa UAE katika vita vya hivi karibuni vya Marekani na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Iran ni sawa na "kusaidia kambi ya ukafiri dhidi ya ndugu Waislamu" na hivyo, "kimsingi ni haramu."
-
Sababu Gani Zinaifanya UAE Ishupalie Vita Dhidi ya Iran?
May 06, 2026 11:21Muungano wa Falme za Kiarabu, UAE au Imarati umechukua msimamo wa waziwazi wa kushupalia vita hususan dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Sudan yazituhumu Imarati na Ethiopia kushambulia uwanja wa ndege wa Khartoum
May 05, 2026 11:41Sudan leo Jumanne imrudisha nyumbani balozi wake nchini Ethiopia kwa mashauriano na kuzituhutumu Ethiopia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa zimehusika na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) katika uwanja wa ndege wa Khartoum.