-
Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa Libya: Imarati inakiuka sheria za kimataifa
May 20, 2020 03:26Mwakilishi wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya (GNA) katika Umoja wa Mataifa amesema: Umoja wa Falme za Kiarabu unakiuka sheria za kimataifa kwa kutuma silaha nchini Libya.
-
Serikali ya mwafaka wa kitaifa ya Libya yataka kukatwa uhusiano na Imarati
May 16, 2020 06:32Mjumbe wa Baraza la Rais la Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa nchini Libya, sambamba na kuashiria ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na uungaji mkono wa Imarati kwa jenerali muasi Khalifa Haftar, ametaka kukatwa uhusiano wa Tripoli na Abu Dhabi.
-
Uturuki: Imarati, Misri na baadhi ya nchi, zimelitumbukiza eneo la Asia Magharibi katika ghasia na machafuko
May 13, 2020 10:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema kuwa maamuzi na hatua mbovu za Imarati, Misri na baadhi ya nchi za Kiarabu na Magharibi, vimelitumbukiza eneo la Asia Magharibi katika ghasia na machafuko.
-
HRW: Shambulizi la 'drone' ya Imarati liliua raia 8 Tripoli, Libya
Apr 30, 2020 03:38Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema shambulizi la ndege isiyo na rubani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) dhidi ya mji mkuu wa Libya, Tripoli mwishoni mwa mwaka jana liliua na kujeruhi raia wasio na hatia.
-
Wanamgambo wa Imarati wajitangazia uhuru kusini mwa Yemen; Answarullah yalaani
Apr 26, 2020 06:56Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amelaani hatua ya wanamgambo wa Umoja wa Falme za Kiarabu ya kujitangazia uhuru huko kusini mwa Yemen na kusema kuwa, hatua hiyo ni kutangaza kujitoa kikamilifu wanamgambo hao katika makubaliano ya Riyadh kati yao na serikali iliyojiuzulu ya Abdu Rabbuh Mansour Hadi.
-
Msuguano baina na UAE na Saudia washtadi kusini mwa Yemen
Apr 26, 2020 03:17Siku chache baada ya kuvunjika mazungumzo baina ya serikali iliyojiuzulu ya Yemen ya Abdrabbuh Mansur Hadi inayoungwa mkono na Saudi Arabia na Baraza la Mpito la Kusini linaloungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu, vibaraka hao wa Imarati wamejitangazia mamlaka ya ndani katika mikoa ya kusini mwa nchi hiyo maskini ya Kiarabu iliyozama kwenye dimbwi la vita.
-
Libya: Watawala wa Imarati ndio wanaosababisha maafa nchini mwetu
Apr 23, 2020 07:08Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa ya Libya amesema kuwa, watawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ndio wanaosababisha maafa nchini Libya kutokana na wanamgambo wake walioko chini ya jenerali muasi Khalifa Haftar kutumia gesi za sumu katika mashambulizi yao.
-
Mamluki wa Saudia na Imarati watishiana vita Yemen
Apr 19, 2020 03:14Kundi la watu wanaopigania kujitenga kusini mwa Yemen linaloungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu limetoa onyo kali la kuingia vitani na mamluki wa Saudi Arabia, huku migawanyiko baina ya pande mbili hizo ikiendelea kupanuka.
-
UAE yanunua mfumo wa makombora wa Israel na kuwapa wapiganaji wa Haftar
Apr 12, 2020 23:08Umoja wa Falme za Kiarabu umenunua mfumo wa kisasa wa makombora kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa ajili ya kuwapa wanamgambo wa kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya (LNA) linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar.
-
Vibaraka wa Imarati wapigana kusini mwa Yemen
Mar 25, 2020 07:53Duru za habari zimeripoti kujiri mapigano makali kati ya wanamgambo vibaraka wa Imarati katika mji wa Aden, kusini mwa Yemen.