Aug 05, 2024 02:31
Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametilia mkazo haki ya kisheria ya Tehran ya kuuadhibu utawala wa Kizayuni; na amelaani na kukemea hatua ya baadhi ya nchi za Ulaya ya kushirikiana na Marekani kuzuia kulaaniwa mauaji ya Kiongozi Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) shahidi Ismail Haniyeh katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.