-
Zaidi ya wagonjwa 83 elfu wa COVID-19 wamepata nafuu nchini Iran
May 08, 2020 19:32Wizara ya Afya, Matibabu na Mafunzo ya Tiba ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa waathiriwa 83 elfu na 837 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata nafuu na afya njema na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Russia yatangaza mshikamano wake na watu wa Iran
May 07, 2020 22:19Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amewatumia barua viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akitangaza mshikamano wake na raia wa nchi hii kutokana na mapambano yao makubwa dhidi ya vikwazo haramu na vya upande mmoja vya Marekani katika mazingira ya sasa.
-
Wanadiplomasia wa EU: Marekani haina haki ya kutaka kurefushwa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran
May 06, 2020 03:31Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema kwa kujiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran, Marekani ilipoteza haki yake ya kutaka kurefushwa vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.
-
Iran yasema madai ya Marekani dhidi yake ni 'mzaha mchungu'
May 06, 2020 03:28Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kuashiria juu ya uhusiano madhubuti baina ya taifa hili na Afghanistan, imekosoa vikali madai ya Marekani dhidi ya Tehran kuhusu tukio la kupoteza maisha raia wa Kiafghani katika eneo la Herat, mpakani mwa nchi mbili hizi.
-
Marekani yawaliwaza kwa medali askari wake waliojeruhiwa katika shambulizi la Iran
May 05, 2020 03:34Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani imewatunuku medali za heshima makumi ya askari wake waliojeruhiwa katika shambulizi kali la Iran la mapema mwaka huu nchini Iraq.
-
Zaidi ya wagonjwa 78 elfu wa COVID-19 wamepona nchini Iran
May 04, 2020 01:31Wizara ya Afya, Matibabu na Mafunzo ya Tiba ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa waathiriwa 78 elfu na 422 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata nafuu na afya njema na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
-
Shamkhani: JCPOA itakufa kikamilifu iwapo vikwazo vya silaha dhidi ya Iran vitarefushwa
May 03, 2020 03:46Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameonya kuwa, iwapo azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakiukwa kwa kuongezwa muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Tehran, basi makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yatakufa daima.
-
Iran: Marekani haina misingi ya kisheria kujifanya mshiriki wa JCPOA
May 03, 2020 03:41Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Taasisi za Kimataifa mjini Vienna amesema jitihada za Marekani za kutaka kuionesha dunia kuwa ingali mshiriki wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hazina misingi ya kisheria.
-
Russia yakosoa msimamo wa kinafiki wa Marekani kuhusu JCPOA na azimio 2231
May 02, 2020 22:01Licha ya kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) mwezi Mei 2018, Marekani imekuwa na msimamo wa kinafiki na kimaslahi kuhusiana na mapatano hayo pamoja na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Makubaliano ya JCPOA; kuanzia kushindwa “mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa” hadi “ndoto za alinacha” za Mike Pompeo
Apr 30, 2020 20:09Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, juhudi za Marekani za kutaka kuongezwa muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran zinakwenda kinyume na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.