-
Iran: Marekani lazima imwachie huru Rais iliyemteka nyara wa Venezuela
Jan 05, 2026 08:04Iran, kwa mara nyingine tena, imekosoa kitendo cha Marekani cha kumteka nyara Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro na mkewe, Cilia Flore, na kueleza kuwa waliotekwa nyara lazima waachiwe huru kama inavyosisitizwa na maafisa na wananchi wa Venezuela.
-
Hizbullah: Iran haijataka chochote kwetu mkabala wa kutusaidia, kutuunga mkono
Jan 04, 2026 07:36Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem amepongeza ustadi wa kijeshi wa aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Luteni Jenerali Qassem Soleimani na kuongeza kuwa, Iran haijataka chochote kutoka kwa harakati hiyo ya Muqawama mkabala wa uungaji mkono wake kwake.
-
Iran yaihutubu UN kuhusu 'mwenendo haramu endelevu' wa Trump
Jan 03, 2026 03:31Iran imeuonya rasmi Umoja wa Mataifa kuhusu "mwenendo haramu endelevu" wa Marekani, kufuatia matamshi ya vitisho ya Rais Donald Trump ambayo Jamhuri ya Kiislamu imeyashutumu na kuyaeleza kama ya uingiliaji wa mambo yake ya ndani na tishio la wazi la utumiaji nguvu.
-
Araghchi amjibu Trump: Vikosi vya Iran viko tayari kujibu mapigo
Jan 02, 2026 23:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amemuonya Rais wa Marekani, Donald Trump dhidi ya kuingilia masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu, akikosoa matamshi yake ya hivi karibuni na kuyaeleza kuwa "yasiyo na busara na hatarishi," na kusisitiza kwamba vikosi vya jeshi la Iran vimejiandaa kikamilifu kulinda mamlaka ya kujitawala nchi hii.
-
Onyo kuhusu matokeo mabaya ya vitisho vya Marekani dhidi ya mpango wa nyuklia wa amani wa Iran
Jan 02, 2026 08:59Tehran imeonya kuhusu matokeo mabaya ya vitisho vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya mpango wa nyuklia wa amani wa Iran.
-
Wairani wamkumbuka na kumuenzi Haj Qassem Soleimani
Jan 02, 2026 07:29Maelfu ya watu kutoka Iran na kote ulimwenguni wamekusanyika katika mji wa Kerman ulioko kusini mwa Iran, kuadhimisha kumbukizi ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.
-
Iran yajibu bwabwaja, vitisho na matamshi ya uingiliaji ya Trump
Jan 02, 2026 06:47Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameonya kwamba, uingiliaji kati wa Marekani katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu utavuruga utulivu wa eneo zima la Asia Magharibi na kuhatarisha moja kwa moja maslahi ya Marekani katika eneo.
-
Iran yatahadharisha kuhusu vitisho vya Marekani dhidi ya maeneo yake ya nyuklia
Jan 01, 2026 08:52Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa mjini Geneva, Uswisi ametahadharisha kuwa hatua ya Marekani ya kuhalalisha vitisho dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii ianahatarisha itibari na hadhi ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).
-
Ujumbe wa wazi kutoka Russia kwa Marekani na Israel; sitisheni vitisho dhidi ya Iran
Jan 01, 2026 06:46Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amekosoa vikali vitisho vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, na kusema jamii ya kimataifa inapinga sera hizo za vitisho.
-
Wizara ya Usalama imewatia mbaroni watu 7 wenye mfungamano na makundi adui yaliyoko US, UK
Jan 01, 2026 03:42Wizara ya Usalama na Intelijensia ya Iran imewatia mbaroni watu saba wanaohusishwa na makundi yenye uadui na Jamhuri ya Kiislamu ambayo yana makao yao Marekani na barani Ulaya.