-
Ujumbe unaokinzana wa Trump kwa Iran
May 30, 2019 21:52Rais Donald Trump wa Marekani siku zote amekuwa na misimamo ya kihasama na kiadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na daima anasisitiza suala la kuzidisha masihinizo dhidi ya Tehran kwa shabaha ya kuilazimisha kukubali matakwa ya Washington.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu; taathira ya nyenzo za mashinikizo za Iran mkabala wa Marekani
May 30, 2019 06:51Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwa mara nyingine tena kuwa kamwe Iran haitafanya mazungumzo na Marekani kwa sababu mazungumzo hayo kwanza, hayana faida yoyote na pili ni kwamba yana madhara kwa taifa la Iran.
-
Jumatano, Mei 29, 2019
May 28, 2019 21:58Leo ni Jumatano tarehe 23 ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1440 Hijria sawa na tarehe 29 Mei mwaka 2019 Miladia.
-
Kuunga mkono Russia ubunifu wa Iran wa kupunguza hali ya taharuki Ghuba ya Uajemi
May 28, 2019 07:00Ili kufikia malengo yake haramu katika eneo la Asia Magharibi na Ghuba ya Uajemi, Marekani daima imekuwa ikieneza chuki dhidi ya Iran yaani Iranophobia, na kwa njia hiyo imeibua hitilafu na mgogoro katika uhusiano wa Iran na majirani zake katika Ghuba ya Uajemi. Pamoja na hayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza kuhusu ulazima wa kuwepo uthabiti katika Ghuba ya Uajemi na hata imewasilisha mpango mpya kuhusiana na hilo.
-
Zarif akimhutubu Trump; Kiongozi Muadhamu ameshatangaza silaha za nyuklia ni haramu
May 27, 2019 23:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumatatu usiku amejibu madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwa eti Iran inafuatilia silaha za nyuklia na kusema, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshatangaza kuwa silaha za nyuklia ni haramu.
-
Iran yataka nchi za Ghuba ya Uajemi ziwe macho kuhusu vitisho vya Marekani
May 27, 2019 10:16Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Sera za Marekani za vikwazo dhidi ya Iran zimehatarisha amani na usalama katika eneo hili zima na hivyo nchi za eneo zinapaswa kuwa macho kuhusu vitisho hivyo."
-
Iran: Hatufanyi mazungumzo ya moja kwa moja, au yasiyo ya moja kwa moja na Marekani
May 27, 2019 04:03Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amepuuzilia mbali madai yaliyoenea hivi karibuni kwamba Tehran inafanya mazungumzo na Marekani kwa shabaha ya kupunguza taharuki baina ya nchi mbili.
-
Rouhani: Mapambano ndiyo njia pekee ya kuwakabili wavamizi
May 27, 2019 02:54Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kuwanyooshea mkono wa pongezi wananchi wa Lebanon kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kukombolewa maeneo ya kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni wa Israel, amesisitiza kuwa muqawama ndiyo njia pekee ya kukabiliana na wavamizi.
-
Spika wa Bunge la Iran akosoa njama za Wamagharibi dhidi ya Wapalestina
May 26, 2019 23:57Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amekosoa vikali njama za nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zilizopewa jina la 'Muamala wa Karne' dhidi ya Wapalestina, huku akitoa mwito wa mahudhurio makubwa katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.
-
Wairaq wafanya maandamano makubwa kulaani siasa za Marekani dhidi ya Iran
May 26, 2019 06:56Maelfu ya raia wa Iraq wamefanya maandamano makubwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ukiwemo mkoa wa Baghdad na Basra wakilalamikia siasa za uhasama za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.