Pars Today
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema mashirika yanayojidai kuwa ya kutetea haki za binadamu katika nchi za Magharibi yamepoteza itibari na uhalali wao kwa kufumbia macho jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Kufuatia shambulio lililowalenga raia wa Pakistan ndani ya Iran, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema Tehran na Islamabad hazitavumilia chokochoko za kuharibu uhusiano wa nchi hizo mbili.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja msingi wa uhusiano wa Tehran na nchi za Kiafrika kuwa ni mungamano wa kiroho baina ya mataifa hayo na kwamba uhusiano huo ni moja ya mihimili mikuu ya siasa za nje za Iran.
Leo ni Jumapili 16 ya mwezi Rajab 1445 Hijria mwafaka na 28 Januari 2024 Miladia.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa jibu la kiuhasama lililotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel mkabala wa hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) linaonyesha namna msingi wa utawala huo ulivyojengwa kwa kutegemea vitendo vya mabavu na ubaguzi; na wakati huo huo unadhihirisha namna utawala huo usivyoheshimu kanuni na sheria za kimataifa.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza mafanikio ya kidiplomasia ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu na kuwataka mawaziri wenzake wa mashauri ya kigeni duniani kuunga mkono hatua hiyo ya Afrika Kusini.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uhusiano wa Iran na Mali pamoja na nchi nyingine za Afrika si wa kisiasa na kidiplomasia tu, bali umejengeka katika msingi wa maslahi ya pande mbili na pande kadhaa.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki zimetia saini hati 10 za ushirikiano kwa lengo la kuzidisha uwekezaji, ushirikiano wa kiuchumi na masuala ya kieneo.
Shughuli ya kuwaaga mashahidi wa shambulizi la kigaidi la Israel nchini Syria imefanyika hapa Tehran kwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu, familia za mashahidi hao na umati mkubwa wa wananchi Waislamu wa Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian anataziwa kuitembelea Misri ndani ya siku chache zijazo, huku utawala wa Kizayuni ukiingiwa na kiwewe kutokana na kuendelea kuimarika uhusiano wa Tehran na Cairo.