-
Iran yatoa jibu kwa barua ya nchi 11 za Kiarabu kwa Katibu Mkuu wa UN
Nov 17, 2016 04:02Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua Katibu Mkuu wa umoja huo kujibu barua iliyotumwa na nchi 11 za Kiarabu kwa Katibu Mkuu huyo na kueleza kwamba: Ni kichekesho kuona tawala ambazo zenyewe ndizo zinazolea na kueneza fikra za misimamo mikali na ukufurishaji katika nchi za Iraq na Syria, sasa zinaituhumu Iran kuwa inaunga mkono ugaidi.
-
Ayatullah Khamenei: Iran haina hukumu yoyote kuhusu uchaguzi wa Marekani
Nov 16, 2016 10:55Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina hukumu ya aina yoyote kuhusu uchaguzi wa rais wa Marekani na kuongeza kuwa, Iran daima imekuwa ikishuhudia uadui kutoka kwa vyama viwili vikuu vya Marekani.
-
Bunge la Marekani larefusha vikwazo dhidi ya Iran, maandamano dhidi ya Trump yanaendelea
Nov 16, 2016 04:20Bunge la Marekani limeendelea kuonesha uadui wake dhidi ya Iran kwa kupasisha muswada wa kurefusha vikwazo dhidi ya Tehran kwa miaka kumi zaidi.
-
Iran yalaani mauaji ya Waislamu nchini Nigeria
Nov 15, 2016 10:11Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani hatua ya Jeshi la Nigeria kuwashambulia na kuwaua Waislamu waliokuwa wakishiriki katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS.
-
Rouhani: Iran na Russia zitaendelea kupambana na ugaidi
Nov 15, 2016 01:06Rais wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu na Russia zitaendelea kuwa na ushirikiano wa kistratajia katika kupambana na ugaidi katika eneo hili la Mashariki ya Kati.
-
Diplomasia ya Russia; kustawisha uhusiano na Iran
Nov 14, 2016 23:20Katika kipindi hiki, Tehran imekuwa ikifikiwa na ugeni wa viongozi na maafisa wa nchi mbalimbali za Ulaya. Wakati László Kövér, Spika wa bunge la Hungary akiwa bado mjini Tehran kwa mazungumzo na mashauriano na maafisa wa Iran juu ya uhusiano wa mabunge ya nchi mbili Mwenyekiti wa Baraza la Shirikisho la Russia Valentina Ivanovna Matvienko, naye pia amewasili Tehran kwa safari rasmi ya kikazi.
-
Mogherini: Trump hana uwezo wa kubatilisha JCPOA
Nov 14, 2016 04:34Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 hayawezi kubatilishwa na serikali moja kwa kuwa yana baraka kamili ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Larijani: Uhusiano wa Iran na Russia unaridhisha mno
Nov 14, 2016 04:29Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema uhusiano wa pande mbili kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Russia ni wa kuridhisha mno.
-
Iran yalaani hujuma ya kigaidi nchini Pakistan
Nov 13, 2016 12:38Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani shambulio la kigaidi lililotokea jana Jumamosi katika mkoa wa Baluchestan nchini Pakistan, ambapo makumi ya watu waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
-
Harakati za Saudi Arabia na Imarati dhidi ya Iran katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Nov 13, 2016 09:05Duru za kisiasa zenye mfungamano na Saudi Arabia kwa siku kadhaa sasa zimeanzisha duru mpya ya harakati za kuzidisha mashinikizo dhidi ya Iran.