-
Makumi ya magaidi wa Daesh waangamizwa mjini Mosul, Iraq
Jul 05, 2017 03:40Mkuu wa Jeshi la Polisi la Shirikisho la Iraq ametangaza habari ya kuangamizwa zaidi ya magaidi 60 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wakati wa kusafishwa eneo la kale la mji wa Mosul, kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Kipindi cha baada ya Daesh nchini Iraq na njama mpya za Marekani
Jul 04, 2017 23:34Katika hali ambayo kundi la kigaidi la Daesh linavuta pumzi zake za mwisho nchini Iraq katika siku hizi za kukaribia mwisho operesheni za kijeshi katika mji wa Mosul na kusafishwa sehemu kubwa ya maeneo hayo na uwepo wa magaidi hao na hivyo kuyafanya macho na masikio ya walimwengu kuelekea katika hatua ya mwisho ya uwepo wa Daesh katika nchi hiyo, duru za kisiasa za nchi hiyo ya Kiarabu zimeripoti habari ya kuweko njama mpya za Marekani katika hatua hiyo.
-
Bunge la Iraq lasherehekea kukombolewa mji wa Mosul
Jul 04, 2017 11:10Wabunge wa Iraq wamefanya sherehe kufurahia ushindi wa hivi karibuni na kukomblewa mji wa Mosul kutoka mikononi mwa magaidi wa kitakfiri wa Daesh. Hatua hiyo imechukuliwa na Bunge la Iraq ili kuonyesha mshikamano wa Bunge na vikosi vya jeshi la nchi hiyo na harakati ya wananchi ya Hashdu Sha'abi.
-
ISIS yawafanya wakimbizi wakazi laki tisa wa Mosul, Iraq
Jul 03, 2017 10:46Waziri wa Uhamiaji wa Iraq amesema kuwa, uvamizi na uharibifu mkubwa uliofanywa na genge la kigaidi la Daesh ambao umelilazimisha taifa zima la Iraq kusimama na kuendesha mapambano ya kuukomboa mji wa Mosul wa kaskazini mwa nchi hiyo, umesababisha zaidi ya wakazi laki tisa wa mji huo kuwa wakimbizi.
-
Buriani dola la "khilafa" bandia la Daesh
Jun 30, 2017 04:21Televisheni ya taifa ya Iraq jana ilitangaza rasmi habari ya kukomeshwa na kuangamizwa kundi la Daesh katika mji wa Mosul nchini humo. Habari hiyo iliyokosha na kufurahisha nyoyo za Wairaq na watu wengi wapenda haki na uadilifu kote duniani ilikuwa hitimisho la dola bandia la khilafa ya mawahabi la Daesh ambalo lilianzishwa Juni 2014 kwa ushirikiano wa chama cha Baathi kilichovunjwa huko Iraq, kwa msaada wa Saudi Arabia na washirika wake.
-
Waislamu wa Kisuni wa Mosul, Iraq wawakaribisha kwa shangwe wapiganaji wa Kishia
Jun 28, 2017 13:40Furaha na shamrashamra zimeshamiri na kuwatawala wakazi wa mji wa Mosul ambao ni wa Waislamu wa Kisuni katika kuwakaribisha wapiganaji wa Kishia wa harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi, kufuatia ushindi mkubwa uliofikiwa hadi sasa dhidi ya wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) mjini humo.
-
Waislamu duniani waungana kuswali na kusherehekea Iddil-Fitri
Jun 25, 2017 23:50Leo Waislamu wa maeneo tofauti duniani wanaungana katika swala ya Iddil-Fitri, baada ya kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa siku 30. Hapa Iran swala ya Iddil-Fitri imeswalishwa kitaifa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, hapa mjini Tehran muda mfupi uliopita.
-
UNESCO yaalani vikali hatua ya Daesh ya kubomoa msikiti wa kihistoria wa al Nuri
Jun 23, 2017 00:04Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limelaani vikali hatua ya kundi la kigaidi la Daesh ya kubomoa Msikiti wa kihistoria wa al Nuri katika mji wa Mosul nchini Iraq.
-
Rouhani: Ugaidi eneo la Mashariki ya Kati ni sehemu ya ajenda ya Israel
Jun 21, 2017 03:14Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema operesheni na harakati za kigaidi zinazoshuhudiwa katika eneo hili la Mashariki ya Kati ni sehemu ya ajenda ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa lengo la kuwashughulisha watu ili wasahau kadhia muhimu ya Palestina.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran inapinga kura ya maoni ya kujitenga eneo moja la Iraq
Jun 20, 2017 12:42Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amepongeza umoja na mshikamano wa makundi yote ya kisiasa na kimadhehebu Iraq katika mapambano dhidi ya ISIS au Daesh na kusema uwepo wa 'Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi' ni tuko muhimu na lenye baraka ambalo ni chanzo cha nguvu nchini Iraq.