Marekani yakiri kuuwa mamia ya raia Syria na Iraq
Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imekiri kuwa, ndege za kivita za nchi hiyo na waitifaki wake zimeuwa mamia ya raia huko Syria na Iraq.
Pentagon imekiri katika taarifa yake kwamba, ndege za kivita za Marekani na waitifaki wake kuanzia mwaka 2014 hadi sasa zimeuwa raia 603 huko Iraq na Syria. Ripoti ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeongeza kuwa, raia 119 wamepoteza maisha katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za nchi hiyo na waitifaki wake kuanzia Aprili 19 hadi Mei 23 mwaka huu pekee na kwamba nusu ya wahanga hao waliuawa katika mji wa Mosul kaskazini mwa Iraq au katika eneo la karibu na mji huo.
Pentagon imedai pia kwenye ripoti yake hiyo kuwa, Marekani imetekeleza oparesheni za anga dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Daesh huko Syria na Iraq.
Wasiwasi umeongezeka hivi kuhusu kuuliwa raia zaidi kufuatia katika mashambulizi ya kijeshi ya muungano unaoongozwa na Marekani huko Mosul Iraq na Syria.
Wakati huo huo ripoti zinaonesha kuwa, takwimu zilizotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) kuhusu idadi ya raia waliouawa huko Iraq na Syria ni za kiwango cha chini kulinganisha na idadi halisi ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo. Muungano huo ulianzishwa mwaka 2014 wakati wa utawala wa Rais Barack Obama kwa madai ya kupambana eti na magaidi wa Daesh huko Iraq na Syria. Ripoti rasmi zinaeleza kuwa, Marekani na baadhi ya nchi waitifaki wake wa Magharibi na Kiarabu ndizo zilizoasisi kundi hilo na nchi hizo zinayapatia misaada ya fedha na silaha makundi ya kigaidi likiwemo hilo la Daesh.