Makumi ya magaidi wa Daesh waangamizwa mjini Mosul, Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31356-makumi_ya_magaidi_wa_daesh_waangamizwa_mjini_mosul_iraq
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Shirikisho la Iraq ametangaza habari ya kuangamizwa zaidi ya magaidi 60 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wakati wa kusafishwa eneo la kale la mji wa Mosul, kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jul 05, 2017 03:40 UTC
  • Makumi ya magaidi wa Daesh waangamizwa mjini Mosul, Iraq

Mkuu wa Jeshi la Polisi la Shirikisho la Iraq ametangaza habari ya kuangamizwa zaidi ya magaidi 60 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wakati wa kusafishwa eneo la kale la mji wa Mosul, kaskazini mwa nchi hiyo.

Televisheni ya al Sumaria News ya nchini Iraq imemnukuu Meja Jenerali Shaker Jodat, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Federali nchini Iraq akisema kuwa, vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vinaendelea na opereseheni za kuyasafisha maeneo yaliyobakia na eneo la kale la mji wa Mosul na kuwaokoa wananchi na raia wa kawaida waliokuwa wamezingirwa kwenye mazingira makugumu sana na magaidi wa Daesh.

Magaidi wa Daesh (ISIS)

 

Kwa mujibu wa Meja Jenerali Shaker Jodat, hadi hivi sasa magaidi wasiopungua 57 wa Daesh wameshaangamiza katika operesheni ya kulisafisha eneo hilo la kale kama ambavyo vikosi vya ulinzi vya Iraq vimekamata mikanda mingi ya mabomu na maghala ya makombora na maroketi.

Wakati huo huo kikosi cha kijasusi cha jeshi la Iraq kimefanikiwa kumtia mbaroni gaidi mmoja hatari zaidi na ambaye alikuwa akisakwa muda mrefu katika eneo la al Adhim mkoani Diyala, mashariki mwa Iraq.

Habari nyingine kutoka nchini Iraq imenukuu duru moja ya mkoa wa Kirkuk wa kaskazini mwa nchi hiyo ikisema kuwa, jeshi la Iraq limefanikiwa kuangamiza kiwanda kikubwa na ghala kubwa zaidi la silaha za genge la kigaidi la ISIS katika eneo la kusini magharibi mwa mkoa huo wa Kirkuk. Habari zinasema kuwa magaidi watano wameangamizwa katika shambulio hilo la jeshi la Iraq na wengine saba kujeruhiwa.