-
MOSSAD: Israel kufungua 'ubalozi wake' nchini Oman
Jul 02, 2019 07:24Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel (MOSSAD) amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unatazamiwa hivi karibuni kufungua Ofisi ya Uwakilishi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala huo katili nchini Oman.
-
Bahrain: Tunataka kuimarisha uhusiano wetu na Israel
Jun 27, 2019 21:59Bahrain ambayo ilikuwa mwenyeji wa eti mkutano wa kiuchumi wa mjini Manama baada ya kuficha kwa muda mrefu uhusiano wake na utawala wa Kizayuni wa Israel, hatimaye imefunguka na kusema kuwa inataka kuwa na amani na kuimarisha uhusiano wake na utawala huo haramu.
-
Utawala wa Israel wakereka baada ya rais wa Chile kuutembelea Msikiti wa Al-Aqsa
Jun 27, 2019 03:36Utawala wa Kizayuni wa Israel umekerwa na hatua ya Rais Sebastián Piñera wa Chile akishirikiana na Idara ya Wakfu ya Kiislamu ya Quds na viongozi wa ngazi ya juu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kuzuru Msikiti wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu.
-
Waziri Mkuu wa Palestina: Wapalestina wanataka uhuru na si sadaka
Jun 25, 2019 22:27Waziri Mkuu wa Palestina amesema kuwa mhandisi na mtayarishaji wa mpango wa Kimarekani wa eti amani ya Mashariki ya Kati wa Muamala wa Karne unaosimamiwa na mkwe wa Rais Donald Trump, Jared Kushner na wenzake hawaelewi kuwa Wapalestina hawataki sadaka bali wanadai haki zao za kuwa huru na kukomeshwa uvamizi wa Israel na udhibiti wa dola hilo haramu wa maisha na uchumi wao.
-
Sheikh Isa Qassim: Trump anataka kuiuza Palestina na matukufu yake
Jun 25, 2019 02:25Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Bahrain, Sheikh Isa Qassim sambamba na kulaani hatua ya utawala wa Manama kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kibiashara linalotazamiwa kuanza leo nchini humo kwa shabaha ya kuzindua mpango wa 'Muamala wa Karne' amesema mpango huo wa Rais Donald Trump wa Marekani unakusudia kuwapokonya Wapalestina haki zao zote na kuuza kila kitu kinachomilikiwa nao yakiwemo maeneo matakatifu.
-
Wanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon, Palestina wasusia 'Muamala wa Karne'
Jun 24, 2019 08:18Wanazuoni na wasomi wa Kiislamu wa Lebanon na Palestina wamelaani njama ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina iliyopewa jina la 'Muamala wa Karne'.
-
Saudia yanunua programu ya kijasusi ya Israel kwa dola milioni 300
Jun 21, 2019 00:10Saudi Arabia imeripotiwa kununua programu ya kufanya ujasusi yenye thamani ya dola milioni 300 kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
SIPRI: Israel ina vichwa 100 vya silaha za nyulklia
Jun 17, 2019 03:21Ripoti mpya ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI) imefichua kuwa, utawala haramu wa Israel unamiliki takriban vichwa 100 vya silaha za nyuklia.
-
Israel kushiriki mkutano wa Marekani dhidi ya Wapalestina, Bahrain
Jun 17, 2019 03:16Utawala wa Kizayuni wa Israel umethibitisha kuwa utashiriki mkutano wa 'kiuchumi wa Manama' nchini Bahrain ulioitishwa na Marekani, wenye lengo la kuzindua 'Muamala wa Karne'.
-
Watunisia waandamana dhidi ya Israel, waiunga mkono Palestina
Jun 16, 2019 02:29Makumi ya wanaharakati wa kisiasa na kijamii wa nchini Tunisia kwa mara nyingine wamefanya maandamano katika barabara za mji mkuu Tunis, kulaani mpango wowote wa kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, sambamba na kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina.