-
Ansarullah: Vita kuu nchini Yemen ni dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni
Jun 15, 2018 02:39Sayydi Abdul-Malik Badreddin al-Houthi, Katibu Mkuu wa harakati ya Kiislamu ya Ansarullah nchini Yemen amesema kuwa, vita kuu inayopiganwa nchini humo ni dhidi ya Marekani na utawala haramu wa Israel na kwamba, wavamizi wengine kama Saudi Arabia, Imarati, Misri nk ni wanasesere katika mikono ya Washington na Tel Aviv.
-
Pigo jingine dhidi ya Marekani katika Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina
Jun 14, 2018 23:50Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika fremu ya kuunga mkono taifa madhulumu la Palestina, limepitisha kwa wingi wa kura azimio la kulaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina na kwa utaratibu huo, Marekani, kwa mara nyingine tena, imepata pigo na kugonga mwamba katika jitihada zake za kulaani Harakati ya Mapambanao ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.
-
Assad: Vikosi vya Israel na Uturuki vilivyoko Syria ni vamizi
Jun 14, 2018 03:26Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel, Uturuki, Marekani na Ufaransa vilivyoko nchi humo ni vikosi vamizi.
-
Nchi 120 katika Umoja wa Mataifa zalaani mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina
Jun 13, 2018 22:17Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio linaloulaumu na kuulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kufanya mauaji dhidi raia wa Kipalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
HRW: Israel inafanya jinai za kivita huko Gaza
Jun 13, 2018 11:14Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya jinai za kivita dhidi ya raia wanaoandamana huko katika Ukanda wa Gaza, Palestina.
-
Ethiopia yakanusha madai ya kuhamishia ubalozi wake Quds Tukufu
Jun 12, 2018 09:28Serikali ya Ethiopia imekadhibisha vikali madai kuwa inapanga kuuhamishia ubalozi wake mjini Quds, kutoka Tel Aviv.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu undumakuwili wa nchi za Magharibi
Jun 11, 2018 06:07Ayatullahil Udhma Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumapili katika mkutano wake na mamia ya wahadhiri wa vyuo vikuu na wasomi kutoka taasisi mbali mbali za utafiti nchini alibainisha nafasi ya juu ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa kimataifa.
-
Mkuu wa Sera za Kigeni EU afuta safari yake Tel Aviv, ongezeko la hitilafu baina ya Ulaya na Israel
Jun 09, 2018 22:20Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amefuta safari yake ya kutembelea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) baada ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kusema hatakutana naye katika safari hiyo.
-
Palestina yaitaka UN ichunguze mauaji yanayofanywa na Israel huko Gaza
Jun 09, 2018 03:18Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa Baraza Kuu la umoja huo kukumbatia azimio linalotaka kuchunguzwa jinai za kutisha zinazoendelea kufanywa na wanajeshi katili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Velayati: Muqawama wa Palestina umeidhoofisha mno Israel
Jun 08, 2018 02:57Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema harakati za muqawama wa Palestina zimeudhoofisha utawala wa Kizayuni, na kuandaa mazingira ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Tel Aviv.