Velayati: Muqawama wa Palestina umeidhoofisha mno Israel
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema harakati za muqawama wa Palestina zimeudhoofisha utawala wa Kizayuni, na kuandaa mazingira ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Tel Aviv.
Ali Akbar Velayati amesema hayo katika ujumbe wa video kwa ajili ya Kongamano la Siku ya Quds lililofanyika jana katika Ukanda wa Ghaza na kuongeza kuwa, miaka 40 baada ya Imam Khomeini MA kutangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds, Wapalestina wamefanikiwa kuvirejesha nyuma vikosi vamizi vya Wazayuni, sanjari na kuzuia kuendelea kujitanua utawala hua haramu katika ardhi Palestina.
Mwanadiplomasi huyo wa Iran amekusha kuwa, uhai wa utawala wa Kizayuni ulipatikana kutokana na vitendo viouvu vya Uingereza na nchi nyingine za Magharibi miaka 70 iliyopita, kwa kutoa Azimio la Balfour.
Katika Azimio la Balfour la mwaka 1917, Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo wa Uingereza Arthur James Balfour, alimwandikia barua ya kumtaarifu Walter Rothschild, mwanasiasa wa Kizayuni na mbunge wa bunge la Uingereza kuhusu mtazamo chanya wa serikali ya London juu ya "kuanzishwa nyumba ya kitaifa kwa ajili ya Waisraeli katika ardhi ya Palestina".
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa ameongeza kuwa, licha ya Wapalestina kusalia wakimbizi katika kipindi hicho cha miaka 70 katika ardhi yao, lakini wameimarisha utambulisho wao katika kipindi chote hicho.
Velayati amebainisha kuwa, hali ya kusikitisha ya baadhi ya serikali za Kiislamu kuunga mkono kisiri jinai za Wazayuni, imempa kiburi Rais Donald Trump wa Marekani, kuwashinikiza Wapalestina kukubali kile alichokitaja kama suluhu ya karne, ya Palestina na Israel.