-
Waasi 44 wauawa na jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jan 26, 2021 03:59Jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati limetangaza habari ya kuua waasi 44 waliokuwa na nia ya kuzingira na kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui sambamba na kuipindua serikali ya Rais Faustin Archange Toudera wa nchi hiyo.
-
Askari 2 wa UN wauawa CAR baada ya mahakama kuidhinisha ushindi wa Touadera
Jan 19, 2021 08:11Genge la waasi limeua wanajeshi wawili wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), masaa machache baada ya Mahakama ya Katiba kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa Disemba mwa uliopita, yaliyompa ushindi Faustin Archange Touadera.
-
Askari mwingine wa UN raia wa Burundi auawa CAR, wawili wajeruhiwa
Jan 16, 2021 09:50Askari mwingine wa Umoja wa Mataifa kutoka Burundi ameuawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na wengine wawili wamejeruhiwa, kitendo ambacho kimelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres.
-
Waasi wafanya mashambulio mawili dhidi ya mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jan 13, 2021 08:19Wanamgambo wa makundi ya waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefanya mashambulio mawili alfajiri ya kuamkia leo katika viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Bangui kwa lengo la kuuteka mji huo.
-
Wapinzani Jamhuri ya Afrika ya Kati wapinga matokeo ya uchaguzi
Jan 06, 2021 04:49Wapinzani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamepinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni, wakidai ulikumbwa na dosari.
-
Rais Touadéra achaguliwa tena kuiongoza Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jan 05, 2021 03:43Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amechaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo kwa kipindi kingine cha pili cha miaka mitano baada ya kutangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Desemba.
-
Askari watatu wa kulinda amani kutoka Burundi wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Dec 26, 2020 03:56Askari watatu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao ni raia wa Burundi wameuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati huku mapigano yakishadidi katika nchi hiyo ambayo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu hapo kesho.
-
Katibu Mkuu wa UN ataka kusitishwa uhasama katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Dec 19, 2020 23:15Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kusitishwa uhasama katika Jamhuri ya Afrika Kati wakati huu nchi hiyo ikikaribia kufanya uchaguzi mkuu.
-
Umoja wa Mataifa waongeza muda wa MONUSCO kubakia DRC
Dec 19, 2020 23:14Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa tume yake ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, kuendelea na shughuli zake nchini humo.
-
Machafuko yashtadi Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kukaribia uchaguzi wa rais
Dec 19, 2020 08:45Kitendo cha kuungana makundi yanayobeba silaha katika kukaribia kufanyika uchaguzi wa rais huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kimeibua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wananchi.