Umoja wa Mataifa waongeza muda wa MONUSCO kubakia DRC
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i65290-umoja_wa_mataifa_waongeza_muda_wa_monusco_kubakia_drc
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa tume yake ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, kuendelea na shughuli zake nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 19, 2020 23:14 UTC
  • Umoja wa Mataifa waongeza muda wa MONUSCO kubakia DRC

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka mmoja kwa tume yake ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, kuendelea na shughuli zake nchini humo.

Azimio lililoandaliwa na Ufaransa limepitishwa na wanachama 14 kati ya 15 wa Baraza la Usalama la Umoja la Mataifa, huku Urusi ikikijizuia kupiga kura.

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO itaendelea na shughuli zake za kulinda amani hadi Desemba 20, 2021", ikiwa na askari na maafisa wa polisi karibu 16,300.

Azimio hilo limeitaka sekretarieti ya Umoja aw Mataifa "kuzingatia zaidi namna ya kupunguza idadi ya askari wa kikosi hicho na kupunguza maeneo ya operesheni zake kulingana na jinsi hali ya usalama inavyoendelea katika nchini humo, hasa katika mikoa ambayo ambapo hakuripotiwi tena vitisho kutoka makundi yenye silaha".

Kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO

 

Baraza la Usalama la Umoja aw Mataifa "linaidhinisha" mpango wa pamoja wa UN-DRC uliowasilishwa mnamo mwezi Oktoba "kujiondoa hatua kwa hatua kwa MONUSCO nchini DRC " kwa lengo la kukabidhi majukumu yanayoshikiliwa na walinda amani kwa vikosi vya DRC, lilisomeka azimio hilo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo hasa wa mashariki mwa nchi hiyo wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO na hata kuandamana wakitaka kuondoka askari hao katika nchi yao.

Harakati za makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo kama za ADF-Nalu la Uganda zimevuruga kabisa usalama katika maeneo hayo na kusababisha raia wengi kulazimika kuyakimbia makazi yao.