-
Umoja wa Mataifa walaani hujuma dhidi ya askari wake CAR
Jul 15, 2020 02:38Umoja wa Mataifa umelaani vikali hujuma iliyofanywa dhidi ya askari wake wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo imepelekea kuuawa askari mmoja wa kulinda amani raia wa Rwanda na wengine wawili kujeruhiwa.
-
Jamhuri ya Afrika ya Kati yapata misaada ya uchaguzi huku hofu ya COVID-19 ikitanda
Jun 17, 2020 11:02Shehena ya tatu ya vifaa vya uchaguzi imewasili Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Vifaa hivyo vimetolewa na Umoja wa Mataifa na wadau wake ukiwemo Muungano wa Ulaya, EU, na ni kwa ajili ya uchaguzi wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika nchini humo mwezi Desemba mwaka huu.
-
Msalaba Mwekundu yaomba msaada wa kupambana na corona CAR + Sauti
Apr 15, 2020 17:55Shirika la Msalaba Mwekundu Jamhuri ya Afrika ya Kati limeyaomba mataifa ya dunia yalisaidie shirika hilo kupambana na maambukizi ya corona nchini humo. Mossi Mwasi na maelezo zaidi…
-
UN yaafiki kuendelea vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati
Feb 01, 2020 12:30Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lilowasilishwa na Ufaransa la kuendelea kuwekewa vikwazo vya ununuzi wa silaha Jamhuri ya Afrika ya Kati.
-
Makumi ya watu wauawa katika mapigano baina ya makundi hasimu CAR
Jan 29, 2020 13:38Mapigano makali yaliyotokea baina ya makundi hasimu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yamesababisha mauaji ya makumi ya watu na kuwalazimisha mamia ya wengine kukimbia nyumba zao.
-
Hali ya utulivu yarejea Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya mapigano + Sauti
Dec 27, 2019 15:48Hali ya utulivu imerejea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui baada ya siku mbili za mapigano baina ya makundi mawili hasimu. Mapigano hayo yamesababisha zaidi ya watu 30 kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Mossi Mwasi na maelezo zaidi…
-
Watu wasiopungua 11 wauawa katika mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati
Dec 27, 2019 02:51Watu wasiopungua 11 wameuawa katika mapigano kati ya wanamgambo na wafanya biashara katika wilaya moja huko Bangui mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
-
Mvua kubwa zazidi kusababisha maafa katika nchi mbalimbali za Afrika + Sauti
Oct 30, 2019 16:41Mvua kubwa zinazonyesha katika nchi za Afrika ya Kati hususan Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya Kati zimesababisha maafa makubwa ya watu wengi kupoteza maisha yao na pia makazi. Kwa maelezo zaidi, tumtegee sikio mwandishi wetu wa Afrika ya Kati. Mosi Mwasi, akiripoti kutoka Brazzaville
-
Wanajeshi 3 waaga dunia katika ajali ya helikopta CAR
Sep 28, 2019 11:53Askari watatu wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) wamepoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea jana Ijumaa.
-
Nduli wawili wa Waislamu CAR wapandishwa kizimbani ICC + Sauti
Sep 19, 2019 18:28Wababe wawili wa kivita wa kundi la Anti-Balaka la Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai za Kivita ICC huko Uholanzi kujibu tuhuma za jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu walizozifanya nchini mwao kati ya mwaka 2013 na 2014 wakati mapigano ya ndani Jamhuri ya Afrika ya Kati yalipopamba moto. Mwandishi wetu Mosi Mwassi na maelezo zaidi…