-
Nduli wawili wa Waislamu CAR wapandishwa kizimbani ICC + Sauti
Sep 19, 2019 18:28Wababe wawili wa kivita wa kundi la Anti-Balaka la Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai za Kivita ICC huko Uholanzi kujibu tuhuma za jinai za kivita na zilizo dhidi ya binadamu walizozifanya nchini mwao kati ya mwaka 2013 na 2014 wakati mapigano ya ndani Jamhuri ya Afrika ya Kati yalipopamba moto. Mwandishi wetu Mosi Mwassi na maelezo zaidi…
-
AU na UN zalaani mapigano mapya Jamhuri ya Afrika ya Kati + Sauti
Sep 15, 2019 16:41Umoja na Mataifa na Umoja wa Afrika zimelaani vikali kitendo cha kuibuka upya mapigano katika mji wa Birao wa kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye mpaka na Sudan Kusini. Mapigano hayo yaliyoyahusisha makundi mawili hasama ya genge la Seleka, yamepelekea makumi ya watu kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Hii ni katika hali ambayo makundi hayo, yalitia saini mkataba wa amani kwenye serikali ya umoja wa kitaifa nchini CAR. Mwandishi wetu Mossi Mwasi na maelezo zaidi...
-
Radiamali ya taasisi za kimataifa kufuatia kushtadi machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Sep 04, 2019 02:40Taasisi za kimataifa zimetaka kukabiliana na ongezeko la hali ya machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
-
Wapinzani CAR walalamikia ukandamizaji wa serikali + Sauti
Jul 19, 2019 06:13Vyama vya upinzani na asasi za kijamii za Jamhuri ya Afrika ya Kati zimeilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kukandamiza maandamano yao katika muda wa mwezi mmoja uliopita. maelezo zaidi yamo katika ripoti ya mwandishi wetu, Mossi Mwasi...
-
Makundi matatu ya waasi yaweka chini silaha zao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jul 18, 2019 07:13Makundi matatu ya wabeba silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamekabidhi silaha zao kwa wawakilishi wa Umoja wa Mataifa.
-
Robo ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wametawanywa na machafuko
Jun 21, 2019 04:36Maelfu ya watu ni wa kimbizi wa ndani ya nchi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na hawawezi kurejea makao kutokana na hali tete ya usalama inayoendelea.
-
CAR yawasaka waliotekeleza mauaji katika jimbo Paoua
Jun 06, 2019 02:34Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) inaendeleza jitihada za kuwasaka na kuwafikisha kizimbani waliotekeleza mauaji ya umati hivi karibuni katika jimbo la Paoua nchini humo.
-
CAR yatangaza maombolezo ya kitaifa baada ya mauaji ya umati
May 24, 2019 08:05Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia Alhamisi baada ya watu zaidi ya 50 kuuawa kwa umati Jumanne karibu na mpaka wa nchi hiyo na Chad.
-
Guterres ataka kuharakishwa utekelezwaji wa makubaliano ya amani CAR
Mar 24, 2019 07:59Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa pande zote husika kutekeleza kwa haraka mapatano ya amani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yaliyotiwa saini katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, siku moja baada ya kuundwa serikali mpya inayoyajumuisha makundi ya wabeba silaha.
-
Sherehe za kutiwa saini makubaliano ya Amani CAR sasa kufanyika Jumanne
Feb 04, 2019 07:55Sherehe za kuanza utekelezaji wa makubaliano ya amani baina ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na makundi 14 yenye silaha zilizopangwa kufanyika jana Jumapili, zimeakhirishwa na sasa zitafanyika kesho Jumanne mjini Khartoum, Sudan. Mwenyeji wa makubaliano hayo yaani serikali ya Sudan imesema kuwa, saini ya mwisho ya makubaliano hayo itatiwa baadaye, ingawa haikusema ni lini hasa.