Robo ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wametawanywa na machafuko
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54245-robo_ya_wananchi_wa_jamhuri_ya_afrika_ya_kati_wametawanywa_na_machafuko
Maelfu ya watu ni wa kimbizi wa ndani ya nchi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na hawawezi kurejea makao kutokana na hali tete ya usalama inayoendelea.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 21, 2019 00:06 UTC
  • Robo ya wananchi wa  Jamhuri ya Afrika ya Kati wametawanywa na machafuko

Maelfu ya watu ni wa kimbizi wa ndani ya nchi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na hawawezi kurejea makao kutokana na hali tete ya usalama inayoendelea.

Kwa mujibu wa taarifa, watu 21,000 wamelazimika kuishi kwenye kambi za Lazare na Mbella zinazohifadhi wakimbizi wa ndani na kusimamiwa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati unaojulikana kama MINUSCA. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura OCHA, asilimia kubwa ya wakimbizi hawa wanatoka katika mji wa Kaga Bandoro.

Shirika hilo linasema robo ya watu wote wa CAR wametawanywa na machafuko na kuishia kuwa wakimbizi. OCHA inasema katika mwaka huu wa 2019, watu milioni 2.9 CAR wanahitaji msaada wa kibinadamu lakini hakunda fedha za kutosha za kuwasaidia.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Machafuko huko Jamhuri ya Afrika ya Kati yalizuka mwaka 2013, baada ya waasi wa Seleka kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, François Bozizé. Baada ya Rais Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi wa Kikristo wenye misimamo ya kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Waislamu, ambapo maelfu ya Waislamu waliuawa na wengine wengi kuwa wakimbizi.