Machafuko yashtadi Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kukaribia uchaguzi wa rais
Kitendo cha kuungana makundi yanayobeba silaha katika kukaribia kufanyika uchaguzi wa rais huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kimeibua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wananchi.
Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kuwa, viongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati leo Jumamosi kwa wakati wa huko wametahadharisha kuwa, makundi ya wanamgambo wenye silaha nchini humo yameungana pamoja.
Viongozi wa makundi matatu makuu ya wanamgambo wanaobeba silaha ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya ardhi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuendesha mashambuli huko kaskazini na magharibi mwa nchi wametangaza kuwa, makundi hayo yameungana pamoja na kuasisi muungano wao.
Katika hali ambayo duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na bunge nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imepangwa kufanyika tarehe 27 Disemba mwaka huu huku wakipinzani wakitahadharisha kujiri udanganyifu mkubwa katika uchaguzi huu; hivi sasa mzingiro wa muda mrefu wa muungano huo unatishia Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo.