-
DRC: Watu 1,500 wameuawa mashariki mwa nchi
Jan 02, 2026 02:47Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema zaidi ya raia 1,500 wameuawa katika ghasia zinazoendelea katika jimbo la Kivu Kusini, mashariki mwa nchi hiyo tangu mapema mwezi Desemba, 2025 mpaka sasa.
-
Ukatili wa kingono dhidi ya watoto nchini Kongo umekithiri na ni wa kimfumo
Jan 01, 2026 02:25Ukatili wa kingono dhidi ya watoto limekuwa jambo la kawaida, la kimfumo na unazidi kuongezeka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).
-
Msimamo wa Uingereza dhidi ya wahamiaji wa DRC; kwa nini London inashadidisha mashinikizo dhidi ya nchi za Kiafrika?
Dec 29, 2025 06:58Uingereza imeibua wimbi kubwa la mijibizo na malalamiko ya ndani na ya kimataifa kwa hatua yake ya kuweka vizuizi vya viza na kupitisha mageuzi makali kwa utoaji hifadhi ya ukimbizi.
-
Waasi wa M23 wamebaki Uvira licha ya kutangaza kuwa tayari kuondoka katika mji huo
Dec 18, 2025 07:25Waasi wa kundi la M23 hawajaondoka katika mji wa Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo licha ya mapema wiki hii kutangaza kuwa wataondoka katika mji huo.
-
M23 yaendelea kuwashikilia mamia ya askari wa Burundi
Dec 16, 2025 04:06Kundi la waasi wa M23 linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda limewakamata mamia ya wanajeshi wa Burundi wakati wa mashambulizi yake ya hivi punde mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa kundi hilo amesema, huku mapigano yakiendelea mashariki mwa DRC.
-
Serikali ya Kongo yatoa hakikisho; yasema haitasalimu amri licha ya hali ya wasiwasi mashariki mwa nchi
Dec 13, 2025 09:52Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Ijumaa ilitoa hakikisho ikieleza kuwa jeshi la nchi hiyo halitasalimu amri" kufuatia kutekwa mji wa Uvira.
-
Waasi wa M23 wadai kuuteka mji wa kiistratejia wa Uvira, mashariki mwa Kongo
Dec 11, 2025 11:58Waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana Jumatano walitoa taarifa wakidai kuuteka mji wa kimkakati wa Uvira, ambao ni kitovu muhimu cha kibiashara karibu na mpaka wa nchi hiyo na Burundi.
-
Mshindi wa Tuzo ya Nobel, Denis Mukwege: Makubaliano ya amani kati ya Kinshasa na M23 ni 'haramu'
Dec 02, 2025 06:23Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Dkt. Denis Mukwege amelaani mchakato wa amani unaoendelea kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23 unaolenga kukomesha mapigano mashariki mwa DRC.
-
Wagonjwa ni kati ya watu karibu 30 waliouawa katika shambulio la waasi mashariki mwa Kongo
Nov 18, 2025 10:58Takriban watu 29, wakiwemo wagonjwa wameuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) ambalo lililenga kituo cha afya na vijiji kadhaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
EU yataka kufunguliwa korido ya kibinadamu mashariki mwa Kongo
Nov 06, 2025 11:09Afisa wa Umoja wa Ulaya ametoa wito kwa pande husika katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufungua koridi ya kibinadamu na kuruhusu kuanza kuingia kwa ndege za misaada ya kibinadamu.