-
Rais Tshisekedi amtuhumu mtangulizi wake kwa kuwaunga mkono waasi
Aug 07, 2024 07:50Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Joseph Kabila ameanzisha mkakati wa kuunganisha makundi yenye silaha na vyama vya kisiasa nchini humo dhidi ya serikali yake.
-
Baraza la Usalama laidhinisha MONUSCO kuipa SADC msaada wa kilojistiki DRC
Aug 07, 2024 03:13Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kuidhinisha kikosi cha kusimamia amani cha umoja huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO kutoa msaada wa kiutendaji na wa suhula na zana za kijeshi kwa ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) nchini DRC.
-
Mahakama ya Nigeria yawatia hatiani wanamgambo 125 wa kundi la kigaidi la Boko Haram
Jul 28, 2024 23:03Mahakama nchini Nigeria imewatia hatiani wanamgambo 125 wa kundi la kigaidi la Boko Haram na wafadhili wa kifedha wa msururu wa makosa yanayohusiana na ugaidi.
-
DRC yamuita balozi wa Uganda kujadili tuhuma za kuunga mkono M23
Jul 21, 2024 07:32Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imemuita balozi mdogo wa Uganda nchini humo, baada ya Umoja wa Mataifa kusema katika ripoti yake kwamba, jeshi la Uganda limewauga mkono waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC.
-
Mapigano baina ya jeshi na wanamgambo yaua watu 50 DRC
Jul 16, 2024 03:49Watu zaidi ya 50 wameripotiwa kuuawa katika mapigano makali baina ya askari wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi moja la wanamgambo magharibi mwa nchi.
-
DRC: Askari wa UN kutoondoka kutokana na 'uvamizi' wa Rwanda
Jul 14, 2024 03:18Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) huenda kikalazimika kuakhirisha mpango wa kuwaondoa wanajeshi wake katika mkoa unaokumbwa na vita wa Kivu Kaskazini kutokana na kuwepo kwa askari wa Rwanda mashariki mwa DRC.
-
Raia 6 wa China na askari 2 wa DRC wauawa mkoani Ituri
Jul 04, 2024 22:46Waasi wa kundi la CODECO wameshambulia mgodi unaohusishwa na China katika jimbo lenye utajiri mkubwa wa dhahabu la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuua raia sita wa China wa wanajeshi wawili wa Kongo.
-
Wanajeshi 25 wahukumiwa kifo Kongo kwa kumkimbia adui
Jul 04, 2024 03:14Jumla ya washtakiwa 31, wakiwemo wanajeshi 27 na wake zao wanne ambao ni raia wa kawaida wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi ya Butembo katika mkoa wa Kivu Kaskazini, karibu na mstari wa mbele wa vita kwa "kutoroka vitani na kumpa nafasi adui".
-
Waasi wa Codeco wauwa raia zaidi ya 20 katika jimbo la Ituri, Kongo
Jun 23, 2024 04:10Waasi kwa jina la Codeco wanatuhumiwa kuua raia zaidi ya 20 katika kijiji kimoja katika jimbo tajiri kwa madini ya dhahabu la Ituri kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Watu 80 wakufa maji katika ajali ya boti magharibi ya DRC
Jun 13, 2024 04:11Watu zaidi ya 80 wameripotiwa kuaga dunia baada ya boti iliyokuwa imewabeba kupinduka na kuzama kwenye maji ya Mto Kwa, magharibi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.