-
UN: DRC inahitaji dola bilioni 1.6 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu
Mar 21, 2019 20:47Umoja wa Mataifa umesema unahitaji msaada wa dola bilioni 1.65 za Marekani kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya msingi na ya kibinadamu ya watu milioni 9 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, walioathiriwa na mapigano.
-
Ajali ya treni yaua na kujeruhi zaidi ya watu 130 DRC
Mar 19, 2019 02:30Ajali ya garimoshi la kusafirishia mizigo iliyotokea siku ya Jumapili katika mkoa wa Kasai wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesababisha kupoteza maisha zaidi ya watu 50 na kujeruhiwa wengine wapatao 80.
-
Rais Felix Tshisekedi wa DRC awaachia huru mamia ya wafungwa wa kisiasa
Mar 14, 2019 10:35Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi amesaini dikrii ya kuwaachia huru mamia ya wafungwa wa kisiasa.
-
UN: Mauaji ya watu zaidi ya 500 DRC ni jinai dhidi ya binadamu
Mar 12, 2019 22:56Umoja wa Mataifa umesema mauaji ya zaidi ya watu 500 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yanaweza kuhesabiwa kuwa jinai dhidi ya binadamu.
-
Ugonjwa angamizi wa tauni waibuka mpaka wa Uganda na DRC
Mar 12, 2019 13:01Ugonjwa angamizi wa tauni umeibuka katika mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo hadi sasa watu kadhaa wanaripotiwa kupoteza maisha.
-
Bemba ataka ICC impe fidia kwa kumfunga miaka 10 bila hatia
Mar 12, 2019 04:26Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean-Pierre Bemba, ambaye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC mwaka jana ilimuondoa hatiani, anaitaka mahakama hiyo ya mjini The Hague nchini Uholanzi impe fidia ya Yuro milioni 68 kwa kutompata na hatia katika kesi ya jinai za kivita iliyokuwa ikimuandama.
-
Guterres ataka kupunguzwa wanajeshi 2000 wa Monusco waliopo Kongo
Mar 10, 2019 10:32Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kupunguzwa wanajeshi elfu mbili wa kikosi cha kulinda amani cha umoja huo waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Monusco).
-
Mshindi wa Tuzo ya Nobel akosoa serikali ya umoja wa kitaifa DRC
Mar 10, 2019 10:17Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ameitaja kama usaliti kwa wananchi, hatua ya Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kukubaliana na mtangulizi wake, Joseph Kabila kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika nchi hiyo.
-
Waasi wa Mai Mai wahujumu kambi ya kutibu Ebola nchini DRC
Mar 09, 2019 11:44Waasi wa kundi la Mai Mai wamehujumu kambi ya kutibu wagonjwa wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kumuua afisa wa polisi kabla ya kutimuliwa na maafisa wa usalama.
-
UN yatafakari kupunguza askari wake wa kulinda amani DRC
Mar 08, 2019 00:06Huenda idadi ya askari wa Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO ikapunguzwa.