Pars Today
Saudi Arabia imeripotiwa kutoa pendekezo kwa siri la kuwa tayari kugharamia ujenzi wa miundombinu yote kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia inayotazamiwa kufanyika Ugiriki na Misri mwaka 2030.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amedai kuwa nyota wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo alipigwa marufuku ya kisiasa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia ya FIFA ya 2022 iliyomalizika hivi karibuni nchini Qatar kwa kuunga mkono Palestina.
Pazia la mashindano ya soka ya Kombe la Dunia lilifungwa rasmi siku ya Jumapili kwa timu ya taifa ya soka ya Argentina kutwaa kombe hilo baada ya kumshinda bingwa mtetezi Ufaransa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kufanyika kwa mafanikio michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar ni jambo la fakhari kwa nchi za Kiislamu.
Timu ya taifa ya soka ya Argentina imetwaa Kombe la Dunia 2022 baada ya kuwasinda mabingwa watetezi Ufaransa kwa mikwaju ya penalti.
Shirikisho la Soka la Morocco limewasilisha mashtaka dhidi ya mwamumuzi wa mechi ya nusu fainali kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Ufaransa katika mashindano ya Kombe la Dunia Qatar 2022.
Wakati tunakaribia siku za mwisho za mashindano ya Kombe la Dunia Qatar 2022, wimbi la uungaji mkono wa watu wa Qatar, Waislamu na wapenda haki kote duniani kwa Palestina, limekuwa la kushangaza na kusisimua sana.
Timu ya taifa ya soka ya Argentina imetinga hatua ya fainali ya mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Qatar baada ya kuibamiza timuu ngumu ya Crotia mabao 3 kwa nunge.
Shirika la Ndege la Morocco, Royal Air Maroc linapanga safari 30 za ndege maalum kuwabeba mashabiki wa soka kutoka Casablanca hadi Doha kwa mchezo wa Jumatano wa nchi hiyo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa.
Timu za soka za taifa za Ufaransa na Morocco zitakutana katika hatua ya nuusu ya fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea huko nchini Qatar.