-
Korea Kaskazini yatupilia mbali takwa la Marekani la kuainisha muda wa kuangamiza silaha zake
Aug 09, 2018 15:00Duru za habari nchini Korea Kaskazini zimetangaza kwamba serikali ya nchi hiyo imetupilia mbali takwa la Marekani la kuainishwa muda wa kuanza kupunguzwa kwa silaha za nyuklia za nchi hiyo.
-
Spika wa Bunge la Iran: Wamarekani hawatekelezi ahadi
Aug 09, 2018 08:00Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Wamarekani wakati wa mazungumzo huzungumza vizuri mno, lakini inapofikia wakati wa utekelezaji hawatekelezi hata ahadi moja waliyoahidi.
-
Rais Rouhani: Marekani haina muamana, haiheshimu ahadi yake yoyote
Aug 08, 2018 14:42Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua ya upande mmoja ya Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, utendaji wa serikali ya Washington katika kipindi hiki chote ulikuwa kwa namna ambayo hii leo, Marekani inatambulika kama nchi isiyo na muamana na isiyotekeleza ahadi yakke yoyote.
-
Korea Kaskazini yalalamikia undumakuwili wa Marekani katika uga wa nyuklia
Aug 06, 2018 12:59Serikali ya Korea Kaskazini kupitia gazeti la chama tawala la Rodong Sinmun, imesema kuwa, hatua ya kurefushwa mkataba wa nyuklia kati ya Marekani na Japan ni kitendo kilicho 'dhidi ya ubinaadamu na dhidi ya amani.'
-
Utayarifu wa China wa kusaidia kustawisha uchumi wa Korea Kaskazini
Aug 06, 2018 01:18Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amesema kuwa, Beijing itaisaidia Korea kaskazini katika kukuza uchumi na ustawi wa nchi hiyo.
-
Korea Kaskazini yapinga mpango wa Japan wa kuweka ngao ya makombora
Jul 30, 2018 04:39Serikali ya Korea Kaskazini im imekosoa hatua ya Japan ya kutaka kuweka ngao ya makombora ndani ya nchi hiyo na kuongeza kuwa Shinzō Abe, Waziri Mkuu wa Japan anakusudia kuibadili nchi yake iwe dola lenye nguvu za kijeshi.
-
Korea Kaskazini yaanza kubomoa kituo cha kurushia makombora cha Sohae
Jul 24, 2018 07:18Duru za habari zimeripoti kwamba Korea Kaskazini imeanza kubomoa kituo cha kurushia makombora cha Sohae katika mji wa Pyongan.
-
Kuendelea siasa za mashinikizo ya Marekani dhidi ya Korea Kaskazini
Jul 22, 2018 13:46Ikiwa ni karibu mwezi mmoja umepita tangu Rais Donald Trump na Kim Jong-un wa Korea Kaskazini wakutane nchini Singapore, Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa, kabla ya kujadiliwa suala la kuondolewa vikwazo dhidi ya Pyongyang, nchi hiyo inatakiwa ipige hatua za kivitendo na kwamba kabla ya hatua hizo kupigwa, mashinikizo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini yataongezeka.
-
China na Russia zapinga takwa la Marekani la kutoiuzia mafuta Korea Kaskazini
Jul 20, 2018 08:18Duru za habari zimearifu kwamba China na Russia zimetupilia mbali pendekezo la Marekani kwa ajili ya kuzuia uuzaji mafuta kwa Korea Kaskazini.
-
Mike Pompeo: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Korea Kaskazini vitaendelea
Jul 19, 2018 07:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa kufikiwa makubaliano kamili ya nyuklia kati ya nchi yake na Korea Kaskazini, kutategemea muda mrefu na kwamba katika kipindi hicho vikwazo vya Washington dhidi ya Pyongyang vitaendelea kuwepo.