Rais Rouhani: Marekani haina muamana, haiheshimu ahadi yake yoyote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i47314-rais_rouhani_marekani_haina_muamana_haiheshimu_ahadi_yake_yoyote
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua ya upande mmoja ya Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, utendaji wa serikali ya Washington katika kipindi hiki chote ulikuwa kwa namna ambayo hii leo, Marekani inatambulika kama nchi isiyo na muamana na isiyotekeleza ahadi yakke yoyote.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 08, 2018 14:42 UTC
  • Rais Rouhani: Marekani haina muamana, haiheshimu ahadi yake yoyote

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua ya upande mmoja ya Marekani ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, utendaji wa serikali ya Washington katika kipindi hiki chote ulikuwa kwa namna ambayo hii leo, Marekani inatambulika kama nchi isiyo na muamana na isiyotekeleza ahadi yakke yoyote.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Ri Yong-ho, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Korea Kaskazini na kueleza kuwa, kupatikana amani na usalama kamili katika Rasi ya Korea ni takwa la Iran na kwamba, matukio katika eneo hilo yana umuhimu mkubwa kwa Tehran.

Rais Rouhani ameashiria uhusiano wa kirafiki wa Tehran na Pyongyang katika kipindi cha miongo iliyopita na kuongeza kuwa, Iran na Korea Kaskazini zina mambo mengi zinayozikutanisha pamoja na zimekuwa na mitazamao inayofanana katika kipindi hiki nyeti na daima zimekuwa zikiungana mkono.

Rais Donald Trump wa Marekani 

Kwa upande wake, Ri Yong-ho, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Korea Kaskazini ameashiria uhusiano wa kirafiki uliopo kati ya nchi yake na Iran pamoja na misimamo ya pamoja ya nchi mbili kuhusiana na masuala ya kieneo na kimataifa na kusema kuwa, siasa za kiistratejia za Korea Kaskazini ni kustawisha zaidi uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kupambana na siasa za kupenda upande fulani kujinufaisha peke yake.

Aidha Ri Yong-ho amesema, hatua ya Marekani ya kujiondoa katika mapatano ya JCPOA haikuwa sahihi na inakwenda kinyume na vigezo vya kimataifa.