Aug 21, 2021 12:55
Ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF inaonyesha kuwa, vijana na watoto bilioni moja duniani hususan wanaoishi katika nchi za Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Nigeria, Guinea, na Guinea-Bissau wanakabiliwa na hatari zaidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, yakitishia afya zao, elimu, na ulinzi, na kuwaweka kwenye hatari ya magonjwa.