Guterres: Mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi umekaribia kubaya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i71156-guterres_mgogoro_wa_mabadiliko_ya_tabianchi_umekaribia_kubaya
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuwa, nchi tajiri duniani zimetumia mabilioni mengi ya dola katika nishati ya kisukuku katika kipindi cha maaambukizi ya corona na kutahadharisha kwamba, mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi umekaribia nukta hatarishi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 11, 2021 22:20 UTC
  • Guterres: Mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi umekaribia kubaya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kuwa, nchi tajiri duniani zimetumia mabilioni mengi ya dola katika nishati ya kisukuku katika kipindi cha maaambukizi ya corona na kutahadharisha kwamba, mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi umekaribia nukta hatarishi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kabla ya kukutana na wakuu wa madola makuu kiuchumi duniani katika kikao cha G-7 huko Uingereza kwamba, kuna wasiwasi kuhusu mabilioni ya dola yanayotumiwa na nchi tajiri katika miradi ya nishati ya visukuku badala ya nishati safi tangu kuanza maambukizi ya corona, licha ya ahadi zilizotolewa kuhusu suala la kuhuishwa uchumi wa kijani.  

Shirika la Nishati Duniani hivi karibuni liliripoti kuwa, sambamba na kuanza tena shughuli mbalimbali duniani kiwango cha joto la dunia kinatazamiwa kuongezeka mwaka huu na kufikia kiwango cha juu zaidi kwa mara ya pili katika historia. 

Wanasayansi hivi karibuni walionya kuwa, kiwango cha joto duniani katika miaka mitano ijayo kinatarajiwa kuongezeka kwa wastani wa nyuzi joto 1.5 na kwenda zaidi ya ilivyokadiriwa katika Makubaliano ya Tabianchi ya Paris.

Makubaliano ya Tabia nchi ya Paris 

Ajenda ya mkutano wa G7 nchini Uingereza ni udiplomasia wa chanjo ya corona, biashara, mazingira na ubunifu wa kukarabati miundomsingi katika nchi zinazostawi.