Feb 25, 2021 03:51 UTC
  • Grossi: Haiwezakani kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa joto duniani bila ya nishati ya nyuklia

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) amesisitiza umuhimu wa nishati ya nyuklia katika uchumi na kutatua mgogoro wa nishati katika siku za usoni.

Rafael Grossi amesema kuwa kwa kuzingatia tatizo la mabadiliko ya tabianchi yanayoukabili ulimwengu na kwa mujibu wa Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi, nchi zote zinapasa kufanya juhudi za kupungua hali ya joto duniani kwa kiwango cha nyuzi joto 1.5 au 2 yaani kiwango cha joto lililokuwepo huko nyuma. Amesema kuwa, suala hilo haliwezi kufanikiwa bila ya nishati ya nyuklia kwa sababu matumizi ya nishati hiyo yatapunguza athari za gesi chafu hadi sifuri.  

Athari za gesi za nyumba ya kijani 

Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa IAEA amesisitiza kuwa, ili kufikia lengo hilo hadi mwaka 2050 hatuwezi kuitupilia mbali nishati ya nyuklia ambayo ni nishati safi.

Rafael Grossi ameongeza kuwa, maafisa husika wa mazingira wanafahamu kuwa, nishati ya nyuklia ni njia nzuri ya utatuzi na inayofaa kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi suala la mabadiliko ya tabianchi.

Wasomi duniani pia wanaamini kuwa, gesi chafu ya nyumba za kijani inapasa kupunguzwa hadi nusu ifikapo mwaka 2030. 

Tags