-
Saiful Islam Gaddafi kukatiza ndoto ya Khalifa Haftar ya kutawala Libya?
Dec 03, 2021 23:07Kurejea kwa Saif al-Islam Gaddafi katika kinyang'anyiro cha urais, kutokana na uamuzi wa Mahakama ya Sabha (kusini mwa Libya), kumechanganya tena karata nchini Libya, hasa kutokana na kukithiri kwa mizozo na mivutano kati yake na Jenerali mstaafu, Khalifa Haftar katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.
-
Le Monde: Sudan inaishi siku zake mbaya zaidi za umwagaji damu tangu baada ya mapinduzi
Nov 18, 2021 23:28Gazeti la Le Monde la Ufaransa limeripoti kuwa Sudan inaishi katika kipindi kibaya zaidi cha ukandamizaji na mauaji ya raia tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 25 Oktoba mwaka huu yaliyoindoa madarakani serikali ya kipindi cha mpito.
-
Cyril Ramaphosa asema, machafuko ya Afrika Kusini 'yamechochewa na kupangwa'
Jul 16, 2021 22:45Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa ghasia kubwa na uporaji ambao umeitikisa nchi hiyo kwa wiki nzima iliyopita vilipangwa na kuchochewa. Ramaphosa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kwanza katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi, Apartheid.
-
Umoja wa Afrika watoa wito wa kurejeshwa amani na utulivu Afrika Kusini
Jul 14, 2021 05:16Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, amelaani kwa nguvu zote vurugu na machafuko makubwa yanayoendelea nchini Afrika Kusini baada ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma kufungwa jela miezi 15 kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi na utumiaji mbaya wa madaraka yake.
-
Afrika Kusini: Watu wasiopungua 45 wameuawa katika maandamano ya kumuunga mkono Zuma
Jul 13, 2021 08:25Idadi ya waliofariki dunia kutokana na vurugu na uporaji unaoendelea Afrika Kusini kwa siku kadhaa sasa imeongezeka hadi 45.
-
AU yashtushwa na machafuko ya baada ya uchaguzi CAR
Feb 21, 2021 04:15Umoja wa Afrika umeeleza wasi wasi wake kutokana na kushtadi machafuko ya baada ya uchaguzi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
-
Majimbo 7 ya Sudan yatangaza hali ya hatari, raia waendeleza maandamano ya kulalamika hali mbaya
Feb 11, 2021 23:12Majimbo saba ya Sudan yametangaza hali ya hatari kufuatia maandamano ya siku kadhaa mtawalia katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo ambapo wananchi wanalalamikia hali mbaya ya maisha na ughali na uhaba wa bidhaa muhimu.
-
ICC: Tuna ushahidi wa kutosha wa kuwafungulia mashtaka maafisa wa Nigeria
Dec 11, 2020 23:58Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC, amesema kuwa, ana ushahidi wa kutosha wa kuweza kuwafungulia mashtaka maafisa wa Nigeria kuhusu mateso na ukandamizaji waliofanyiwa wananchi wa nchi hiyo.
-
Buhari ataka kukomeshwa maandamano, machafuko yaendelea Abuja
Oct 23, 2020 06:58Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ametoa wito wa kukomesha machafuko na maandamano yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kufuatia mauaji ya raia waliokuwa wakiandamana kupinga ukatili wa polisi.
-
Watu 10 wauawa katika machafuko ya baada ya uchaguzi Guinea
Oct 22, 2020 00:14Kwa akali watu 10 wameuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, huku taifa hilo likiendelea kusubiri kwa hamu na shauku kuu matokea ya uchaguzi huo wa Oktoba 18.