-
Mripuko watokeo katika kiwanda cha kusafisha mafuta mashariki mwa Saudia
Oct 16, 2019 08:15Shirika la Kitaifa la Mafuta nchini Saudi Arabia ARAMCO limetangaza kutokea mripuko katika kituo cha kusafisha mafuta, mashariki mwa nchi hiyo.
-
Reuters: Baadhi ya wanafamilia ya kifalme Saudia wanataka Bin Salman awekwe kando, ami yake ashike madaraka
Oct 03, 2019 04:27Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa, baadhi ya wanafamilia ya kifalme inayotawala Saudi Arabia na wafanya biashara wakubwa wa nchi hiyo wameeleza kuvunjwa moyo na uongozi wa mrithi wa ufalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman baada ya hujuma na mashambulizi makali ya wapiganaji wa harakati ya Ansarullah wa Yemen dhidi ya vituo na taasisi za kuzalisha mafuta mwezi uliopita.
-
'Kushambuliwa vituo vya mafuta vya Saudia, kunabainisha udhaifu na kushindwa kwa Riyadh'
Sep 17, 2019 07:55Mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya Magharibi mwa Asia amekadhibisha madai yaliyotolewa kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imehusika katika shambulizi dhidi ya taasisi za mafuta za Saudi Arabia na kusema kuwa, shambulizi hilo kwenye taasisi hizo limeonyesha udhaifu na kushindwa kwa Wasaudi.
-
Jitihada za Trump za kudhibiti bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa
Sep 16, 2019 04:55Mashambulizi yaliyofanywa na wanamapambano wa Yemen dhidi ya taasisi za mafuta za Saudi Arabia na kupelekea kupungua nusu ya uzalishaji wa mafuta wa nchi hiyo na kuvuruga masoko ya kimataifa, yamekabiliwa na msimamo wa kukurupuka wa serikali ya Washington.
-
Sekta ya mafuta ya Iran inaendelea kustawi licha ya vikwazo vya Marekani
Sep 14, 2019 07:09Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema sekta ya mafuta na gesi ya taifa hili inaendelea kustawi na kuimarika licha ya vikwazo vya kidhalimu vya Marekani.
-
Mfalme wa Saudia amteua mwanae kuwa waziri wa nishati
Sep 08, 2019 03:16Mfalme wa Saudi Arabia amemfuta kazi waziri wa nishati Khalid Al-Falih na kumteua mwanae kuchukua nafasi hiyo.
-
Novak: Russia kuwekeza zaidi katika sekta ya mafuta ya Iran
Sep 06, 2019 03:24Waziri wa Nishati wa Russia amesema kuwa nchi yake inachunguza uwezekano wa kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa mafuta nchini Iran.
-
Baada ya kushambuliwa na jeshi la Yemen, Saudia yalazimika kupandisha bei ya mafuta, wananchi wakasirika
Jul 14, 2019 06:01Shirika kubwa zaidi la mafuta la Saudi Arabia la Aramco ambalo hivi karibuni lilipata hasara kubwa baada ya kushambuliwa na ndege zisizo za rubani za jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen, limelazimika kupandisha bei ya mafuta nchini humo ili kufidia hasara hizo kutoka kwenye mifuko ya wananchi.
-
Zarif: Liwe liwalo, Iran itaendelea kuuza mafuta yake nje
Jul 14, 2019 02:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vikwazo haramu vya Marekani dhidi ya taifa hili na kusisitiza kuwa, Tehran itaendelea kuyauza mafuta yake nje ya nchi bila kubabaishwa na chochote.
-
China yajibu vitisho vya Marekani vya kuitaka Hong Kong izizuie meli za mafuta za Iran
Jun 02, 2019 02:28Serikali ya China imetupilia mbali vitisho vya Marekani vya kuitaka kuziwekea vikwazo meli za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zisitie nanga na kutoa huduma zake katika bandari ya Hong Kong.