Mripuko watokeo katika kiwanda cha kusafisha mafuta mashariki mwa Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56658-mripuko_watokeo_katika_kiwanda_cha_kusafisha_mafuta_mashariki_mwa_saudia
Shirika la Kitaifa la Mafuta nchini Saudi Arabia ARAMCO limetangaza kutokea mripuko katika kituo cha kusafisha mafuta, mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 16, 2019 08:15 UTC
  • Mripuko watokeo katika kiwanda cha kusafisha mafuta mashariki mwa Saudia

Shirika la Kitaifa la Mafuta nchini Saudi Arabia ARAMCO limetangaza kutokea mripuko katika kituo cha kusafisha mafuta, mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, kwa akali watu wawili ambao ni wafanyakazi wa kituo hicho cha kusafisha mafuta wamefariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mripuko huo umetokea katika kituo cha Al Jubail kilichopo mkoa wa Mashariki nchini humo.

Shirika la Mafuta la Saudia ARAMCO

Hii ni katika hali ambayo baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza kuwa watu 18 wameuawa na kujeruhiwa katika tukio hilo. Hata hivyo shirika hilo la kitaifa la mafuta halijatoa taarifa zaidi juu ya chanzo cha mlipuko huo kwenye kituo hicho. Itakumbukwa kuwa baada ya wanamapambano wa Yemen kushambulia na kuteketeza taasisi za mafuta za Saudi Arabia mwezi uliopita, dhirika la ARAMCO lilikumbwa na mgogoro mkubwa wa fueli kiasi cha kulazimika kununua nishati hiyo kutoka India ambayo nayo inanunua mafuta kutoka Iran.