-
Askari polisi aliyemuua Mmarekani mweusi, George Floyd apatikana na hatia
Apr 21, 2021 05:59Derek Chauvin, afisa mzungu wa polisi wa Marekani ambaye alimuua kikatili Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd na kuzusha maandamano makubwa ya kupinga ubaguzi wa rangi dunia nzima hatimaye amepatikana na hatia katika mashitaka yote ya mauaji yaliyokuwa yakimuandama.
-
Waziri Mkuu wa zamani wa Kuwait azuiwa kusafiri nje ya nchi kwa tuhuma za ufisadi
Mar 30, 2021 08:02Mahakama ya Mawaziri inchini Kuwait imempiga marufuku kusafiri nje ya nchi Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo. Jaber al Mubarak al Hamad all Sabah anakabiliwa na kesi ya ufisadi wa mamia ya mamilioni ya dinari za mfuko wa hazina wa jeshi la nchi hiyo.
-
Mahakama ya Katiba ya Niger 'yabariki' ushindi wa Mohamed Bazoum
Mar 22, 2021 11:13Mahakama ya Katiba ya Niger imeidhinisha ushindi wa matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi mgombea wa chama tawala cha PNDS, Mohamed Bazoum.
-
Kesi ya uchaguzi; Mahakama ya Juu ya Uganda yakataa ombi la Wine
Feb 10, 2021 02:31Mahakama ya Juu ya Uganda imetupilia mbali ombi la mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, la kutaka kufanyia marekebisho faili lake la kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi Rais Yoweri Museveni.
-
Mmishonari wa Marekani afungwa miaka 15 kwa kunajisi mayatima Kenya
Feb 05, 2021 11:45Raia wa Marekani ambaye alikuwa anafanya kazi kama mmishonari nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 15 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi mabinti mayatima.
-
Kabuga afikishwa katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa, asema hana hatia
Nov 12, 2020 04:21Mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Felicien Kabuga jana Jumatano alifikishwa katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania ambapo alisisitiza kuwa hana hatia katika mashitaka ya jinai yanayomkabili.
-
Ushindi mwingine wa Maduro baada ya Mahakama ya Rufaa ya Uingereza kutoa hukumu kwa maslahi ya Venezuela
Oct 07, 2020 07:50Tangu kuanza mgogoro wa uchaguzi nchini Venezuela, Umoja wa Ulaya na nchi kubwa za Ulaya zimechukua msimamo sawa na wa Marekani dhidi ya Rais Nicolas Maduro wa Venezuela. Baada ya kinara wa wapianzani, Juan Guaido kushindwa katika uchaguzi na kisha kujitangaza rais mnamo Januari 23, 2029, nchi za Ulaya ikiwemo Uingereza, zimekuwa zikimuunga mkono kiongozi huyo wa upinzani.
-
EACJ yatupilia mbali faili la ukomo wa urais nchini Uganda
Sep 30, 2020 13:41Mahakama ya Uadilifu ya Afrika Mashariki (EACJ) imetupilia mbali faili lililowasilishwa kwake la kupinga uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Uganda, wa kuidhinisha mabadiliko ya katiba yalioondoa ukomo wa umri wa kugombea urais katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
-
Mashirika yakosoa hukumu 'nyepesi' dhidi ya askari walioua raia Cameroon
Sep 23, 2020 01:34Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali hatua ya mahakama moja nchini Cameroon kuwapa adhabu laini wanajeshi waliopatikana na hatia ya kuua raia akiwemo mtoto mdogo.
-
Baraza la Katiba Ivory Coast lamuidhinisha Outtara kugombea muhula wa 3 wa urais
Sep 15, 2020 03:35Baraza la Katiba la Ivory Coast limemuidhinisha Rais Alassane Outtara kugombea muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwezi ujao.