-
Makabiliano ya kijeshi yasiyo ya kawaida kati ya Russia na Marekani katika anga ya Bahari Nyeusi
Mar 16, 2023 00:45Kituo cha kamandi ya Marekani barani Ulaya kimetangaza kuwa Jumanne asubuhi, ndege ya kivita ya Russia aina ya Sukhoi Su-27 iligongana na ndege isiyo na rubani (droni) ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper katika anga ya Bahari Nyeusi, na kupelekea droni hiyo kuanguka kwenye maji ya kimataifa.
-
National Review: Makubaliano ya Iran-Saudia ni kikwazo kikubwa kwa sera za kigeni za Marekani
Mar 15, 2023 08:51Jarida la National Review limeandika kuwa: Makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia ambayo yalifikiwa kwa upatanishi wa China ni kushindwa kukubwa kwa malengo ya sera za nje za Marekani katika eneo la Mashariki mwa Asia.
-
Droni ya US yaanguka ikidaiwa kugongana na ndege ya kivita ya Russia, Moscow yakanusha
Mar 15, 2023 03:53Jeshi la Marekani limedai kuwa ndege ya kivita ya Russia ilinasa propela ya ndege moja ya kijasusi isiyo na rubani ya nchi hiyo na kuifanya ianguke kwenye Bahari Nyeusi jana Jumanne katika makabiliano ya kwanza ya moja kwa moja kati ya madola hayo mawili tangu Russia ilipoanzisha operesheni za kijeshi nchini Ukraine mwaka mmoja uliopita.
-
FBI: Uhalifu wa chuki dhidi ya wasio wazungu umeweka rekodi Marekani
Mar 14, 2023 09:27Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) imesema kuwa uhalifu wa chuki dhidi ya watu wa mbali tofauti uneongezeka kwa kasi nchini humo na kuweka rekodi ya juu zaidi.
-
Kuvunjwa rasmi mpango wa INSTEX; nembo ya kukiukwa ahadi za Ulaya mkabala wa utekelezaji wa JCPOA
Mar 11, 2023 08:15Troika ya Ulaya inayoundwa na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza juzi Alhamisi ilitangaza katika taarifa yake kuwa imesitisha mfumo kwa jina la mpango wa mabadilishano ya kifedha na kibiashara "INSTEX" uliouanzisha mwaka 2019 kwa ajili ya kulinda biashara na Iran mkabala wa vikwazo vya Marekani.
-
Saudia yaiomba US iisaidie mpango wake wa nyuklia mkabala wa kuanzisha rasmi uhusiano na Israel
Mar 10, 2023 07:03Saudi Arabia imeiomba Marekani iisaidie katika mpango wake wa kurutubisha madini ya urani ili mkabala wake Riyadh itangaze rasmi kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Wall Street linalochapishwa nchini Marekani.
-
US yaziwekea vikwazo taasisi 39 kwa kuisaidia Iran 'kukwepa' vikwazo vya kifedha
Mar 10, 2023 04:06Marekani imetangaza kuyawekea vikwazo makumi ya mashirika kwa tuhuma za kuisaidia Iran kukwepa vizingiti vya Washington vya kuiweka Tehran nje ya mfumo wa kimataifa wa fedha.
-
China yaikosoa vikali Marekani
Mar 09, 2023 04:25Rais Xi Jinping wa Uchina, amehutubu kwenye mkutano wa mwaka wa chama tawala cha Kikomunisti, ambapo ameishambulia vikali Marekani na kusema: Washington inaongoza kampeni ya "kuzuia, kuzingira na kuikandamiza" China.
-
Kampuni za silaha za US zashtakiwa kwa jinai za kivita Yemen
Mar 08, 2023 23:04Mashirika ya kuzalisha silaha ya Marekani yamefunguliwa mashitaka yakituhumiwa kusaidia na kuwa 'mshiriki' wa jinai za kivita nchini Yemen.
-
Mzozo katika kikao cha G20
Mar 06, 2023 23:01Kikao cha kundi la G20 ambacho kiliitishwa kwa kutiliwa mkazo suala la vita vya Ukraine, kimedhihirisha mzozo na hitilafu kubwa zilizopo baina ya nchi wanachama katika masuala tofauti ya kisiasa na kiuchumi kiasi kwamba kikao hicho kilimalizika bila ya kufikiwa makubaliano yoyote.