Uchunguzi wa maoni: Thamani za maadili nchini Marekani zinazidi kuporomoka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i98642-uchunguzi_wa_maoni_thamani_za_maadili_nchini_marekani_zinazidi_kuporomoka
Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa asilimia 83 ya Wamarekani wanaamini kuwa, thamani za maadili katika nchi hiyo zimedhoofika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 11, 2023 04:25 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Thamani za maadili nchini Marekani zinazidi kuporomoka

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa asilimia 83 ya Wamarekani wanaamini kuwa, thamani za maadili katika nchi hiyo zimedhoofika.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo  asilimia 83 ya Wamarekani wanahisi kuwa, kwa ujumla thamani za maadili katika nchi yao ni "dhaifu" huku asilimiana zinazidi kuporomoka kila siku. Kiwango hiiki ni kikubwa mno ikiliinganishwa na miaka mitano iliyopita.

Aidha kiwango hicho ni ongezeko la asilimia 16 ikilinganishwa na mwaka juzi 2021.

Mnamo mwaka wa 2018, asilimi 49 ya raia wa Marekani walieleza kwamba, thamani za kimaadili katika nchi yao ni dhaifu, asilimia ambayo ilionekana kuwa kiwango cha juu zaidi.

Uchunguzi huo wa maoni ulioendeshwa na taasisi ya Gallup umebaini kuwa ni asilimia moja tu ya Wamarekani wanahisi thamani za maadili katika nchi hiyo ni za hali "bora" na asilimia 12 wanahisi ni za hali "nzuri".

Japokuwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita taasisi ya Gallup imekuwa ikibaini ongezeko la mitazamo hasi kuhusu hali ya thamani za kimaadili nchini Marekani, lakini kiwango cha sasa cha kudhoofika kwa thamani hizo kimeweka rekodi ambayo haijawahi kufikiwa.

Katika uchunguzi wake huo iliofanya, Gallup iliwataka waliotoa maoni yao waeleze pia matatizo makubwa zaidi yanayodhoofisha thamani za maadili ndani ya jamii ya Marekani, ambapo asilimia tano hadi nane ya watu wazima waliobainisha mitazamo yao wametaja ubaguzi wa rangi, watu kutokuwa na imani ya dini, kukosekana tabia njema, mtu kujihisi yeye ndiye mwenye haki na watu kutojali kufunga ndoa.