-
Iran: Hatuogopi Trump akibaki wala hatutasisimuka Biden akiingia madarakani
Nov 11, 2020 04:23Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria matukio ya sasa ya uchaguzi wa rais nchini Marekani na kusema: "Hatuogopi iwapo Trump atabakia na wala hatutasisimuka iwapo Biden ataingia madarakani. Tunachukua maamuzi kwa mujibu wa maslahi yetu."
-
Ujenzi haramu wa vitongoji Palestina umeongezeka maradufu katika utawala wa Trump
Nov 11, 2020 00:43Kundi liitwalo "Amani Sasa" lililoko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel limetangaza kuwa, ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina katika kipindi cha miaka minne ya urais wa Donald Trump nchini Marekani umeongezeka maradufu.
-
Kuuzuliwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani; pigo jingine kwa serikali inayotetereka ya Trump
Nov 10, 2020 23:07Rais Donald Trump wa Marekani ambaye alishika hatamu za uongozi wa nchi hiyo akitokea nje ya mzunguko wa kisiasa, katika uga wa timu yake ya uongozi pia amekuwa na utendaji wa ajabu na ambao haujazoeleka.
-
Trump amfuta kazi Waziri wa Ulinzi, wasomi waonya dhidi ya hatua za rais huyo wa US
Nov 10, 2020 04:40Katika hali ambayo mgogoro unaendelea kutotoka nchini Marekani baada ya Joe Biden kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais huku Donald Trump akipinga matokeo hayo kwa madai kuwa uchaguzi uligubikwa na wizi wa kura, rais huyo anayeondoka wa US amempiga kalamu nyekundu Waziri wa Ulinzi, Mark Esper.
-
Takwa la harakati ya Black Lives Matter kwa Joe Biden
Nov 10, 2020 04:32Ukatili mkubwa na ubaguzi wa rangi wa kimfumo dhidi ya watu weusi daima vimekuwa miongoni mwa sifa kuu za jamii ya Mareikani tangu nchi hiyo ilipoasisiwa. Wamarekani weusi wamekuwa wakikumbana na sulubu na mashaka mengi ya aina mbalimbali za ubaguzi na ukatili licha ya miaka mingi ya mapambano ya kupigania haki zao.
-
Rais Rouhani: Serikali mpya ya Marekani irekebishe sura yake mbaya katika mahusiano na nchi nyingine
Nov 10, 2020 08:28Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa serikali mpya ya Marekani inapaswa kufanya marekebisho katika mienendo yake isiyo ya kibinadamu na nchi nyingine za dunia.
-
Uwezekano wa Biden kuendeleza sera za kivita za Marekani
Nov 10, 2020 01:15Afisa wa zamani wa Shirika la Usalama na Ushirikiano la Ulaya (OSCE) ametahadharisha kuwa, kwa kuzingatia historia ya chama cha Democrat, kuna uwezekano mkubwa kuwa sera za kivita za Marekani zitaendelea wakati wa urais wa Joe Biden.
-
Black Lives Matter yamtaka rais mteule wa Marekani kujali maisha ya Wamarekani weusi
Nov 09, 2020 08:35Harakati ya Black Lives Matter imemwandikia barua rais mteule wa Marekani Joe Biden na makamu wake Kamala Harris ikiwataka wayape kipaumbele matakwa ya Wamarekani weusi.
-
Mke wa Trump, Melania amtaka mumuwe akubali kushindwa katika uchaguzi wa rais
Nov 09, 2020 03:41Mke wa Rais Donald Trump wa Marekani amemtaka mumuwe akubali kushindwa mkabala wa mgombea wa chama cha Democratic, Joe Biden katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 3 mwezi huu.
-
Makundi ya Kipalestina: Msimamo wa uhasama wa Marekani kuhusu Palestina haubadiliki
Nov 09, 2020 00:58Makundi ya Kipalestina yametangaza kuwa kuingia madarakani Joe Biden hakutabadili msimamo wa kiuhasama wa Marekani kuhusu kadhia ya Palestina.