Iran: Hatuogopi Trump akibaki wala hatutasisimuka Biden akiingia madarakani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64555-iran_hatuogopi_trump_akibaki_wala_hatutasisimuka_biden_akiingia_madarakani
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria matukio ya sasa ya uchaguzi wa rais nchini Marekani na kusema: "Hatuogopi iwapo Trump atabakia na wala hatutasisimuka iwapo Biden ataingia madarakani. Tunachukua maamuzi kwa mujibu wa maslahi yetu."
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Nov 11, 2020 04:23 UTC
  • Iran: Hatuogopi Trump akibaki wala hatutasisimuka Biden akiingia madarakani

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria matukio ya sasa ya uchaguzi wa rais nchini Marekani na kusema: "Hatuogopi iwapo Trump atabakia na wala hatutasisimuka iwapo Biden ataingia madarakani. Tunachukua maamuzi kwa mujibu wa maslahi yetu."

Sayyid Abbas Araqchi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulkia masuala ya kisaisa amesema: 'Mimi kama mtaalamu wa uhusiano wa kimataifa siwezi kutumia ibara bora zaidi kuliko ile iliyotumiwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu uchaguzi wa Marekani: Uchaguzi  huu unavutia macho na mazingatio ya walimwengu."

Ameongeza kuwa, nchi ambayo inadai kuwa na demokrasia kubwa zaidi duniani na inatawaliwa kwa misingi kongwe ya demokrasia imejipata katika hali ile ile ambayo imekuwa ikizituhumu nchi zingine kuhusika nayo. Kambi zote zinatuhumiana kuhusu kuhusika katika wizi wa kura na kwamba uchaguzi wote una ufisadi kutokana na madai ya wizi wa kura."

Sayyid Abbas Araqchi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje

Araqchi ameendelea kusema kuwa: "Uchaguzi wa Marekani umeonyesha ukweli mwingine kuhusu kugawanyika jamii ya Marekani. Hivi sasa Marekani imefika katika hatua ambayo imegawanyika katika pande mbili sawa na pande zote mbili zinashindana na haziwezi kustahamiliana." Ameongeza kuwa, Trump, amepata uungaji mkono wa karibu asilimi 50 ya Wamarekani pamoja na kuwa ana sifa nyingi mbaya ikiwa ni pamoja na utumiaji mabavu na kukiuka sheria. Amesema kwa kuzingatia kuwa karibu nusu ya Wamarekani wamempigia kura akiwa na sifa hizo mbaya kuna haja ya kufanyika utafiti kuhusu jambo hilo kwani yanayojiri Marekani yanaweza kuwa hatari kwa duniani.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Trump akienda au asipoenda kitakachobakia ni idiolojia ya Kitrump ya kujiona bora kuliko wengine wote duniani na kupuuza ushirikiano wa kimataifa. Amesema idiolojia hii inafuatwa na asilimia 50 ya raia wa Marekani na nukta hiyo ni ishara kuwa watawala wa Marekani wameiongoza jamii ya nchi hiyo katika maangamizi.